2025
Mzima Kiroho katika Yeye
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Mei 2025


Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Mzima Kiroho katika Yeye

Dondoo

alt text

Pakua PDF

Bwana Mponyaji ataponya mateso yetu yote—ya kimwili na kihisia—katika wakati Wake. Lakini katika kusubiri kuponywa, mtu anaweza kuwa mzima? …

Imani katika Yesu Kristo huzaa tumaini. Ninapata tumaini katika kujitahidi kuwa mzima—ukamilifu uliozaliwa kwa imani katika Yesu Kristo. Imani katika Yeye huongeza tumaini langu kwa ajili ya uponyaji, na tumaini hilo huimarisha imani yangu katika Yesu Kristo. Ni mzunguko wenye nguvu. …

Kuwa mzima inamaanisha kuwa mkamilifu na mzima. Kama vile wanawali watano wenye busara ambao walikuwa na taa zao zilizojaa mafuta wakati bwana harusi alipokuja, tunaweza kukamilishwa kupitia Yesu Kristo wakati tunapojaza taa zetu kwa mafuta ya kustawisha ya uongofu Kwake. …

Tumeamriwa kushiriki nuru Yake. Basi endeleeni kujaza taa zenu kwa mafuta ya uongofu katika Yesu Kristo na kuweni tayari kuzifanya taa zenu ziwake kwa uangavu. Kisha acheni nuru hiyo iangaze. Tunaposhiriki nuru yetu, tunaleta faraja ya Yesu Kristo kwa wengine, uongofu wetu Kwake unaongezeka, na tunaweza kuwa wakamilifu hata wakati tunasubiri uponyaji. Na tunapoacha nuru yetu iangaze kwa uangavu, tunaweza kuwa na furaha hata wakati tunaposubiri. …

Akina dada na akina kaka, jibu ni ndiyo, tunaweza kuwa wazima kiroho, hata wakati tunasubiri uponyaji wa kimwili na kihisia. Ukamilifu si lazima umaanishe urejesho kimwili na kihisia katika maisha haya. Kukamilishwa ni tunda la imani katika Yesu Kristo na uongofu kwa Yesu Kristo na kuacha nuru ya uongofu huo iangaze.