Kikao cha Jumamosi Jioni
Na Tunazungumza Kuhusu Kristo
Dondoo
Manabii wanaoishi katika siku zetu—wanaopokea ufunuo kutoka kwa Mungu wa kutufundisha na kutuongoza—wanazidi kutualika kuja kwa Kristo. … Tungeweza kutaja mifano mingi ya marekebisho na maboresho yaliyotangazwa na Urais wa Kwanza ambayo yamesanifiwa ili kutufokasi juu ya Yesu Kristo. …
Acha tuangalie kwa makini athari za baadhi ya hizi. Kwanza, ishara ya Kanisa.
… Ishara hii inaakisi ukweli kwamba Kristo yupo katikati ya Kanisa Lake na anapaswa kuwa kitovu cha maisha yetu. …
… Ishara hii ni uwakilishi wa kuonekana wa upendo wa Mwokozi Yesu Kristo na ukumbusho endelevu wa Kristo aliye hai. …
Sasa acha tutafakari umuhimu wa Pasaka. … Kwa kifupi, tumehimizwa kuhamia kwenye sherehe ya juu na takatifu ya Pasaka. …
Pasaka inaturuhusu kuheshimu vyote dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo na Ufufuko halisi na wa furaha kwake. …
… Wakati inaonekana kuwa na mwenendo unaokua miongoni mwa wanatheolojia mbalimbali wa Kikristo kutazama Ufufuo katika maneno ya kistiari na ishara, tunathibitisha mafundisho yetu kwamba “Ufufuko unamaanisha kwamba wote ambao wamewahi kuishi watafufuliwa, na Ufufuo ni halisi.” … Yesu Kristo alivunja kamba za kifo kwa kila nafsi iliyo hai. …
Katika kuhitimisha, ninashuhudia kwamba wote wanaokubali mialiko kutoka kwa nabii wetu anayeishi na washauri wake kwa dhati kukumbuka matukio matukufu ambayo huwakilisha Pasaka watapata kwamba muungano wao na Yesu Kristo unakua imara zaidi.