Kikao cha Jumapili Asubuhi
Misaada ya Kiungu kwa ajili ya Maisha ya Duniani
Dondoo
Bila shaka, msaada wenye nguvu zaidi wa Mungu ulikuwa kumtoa Mwokozi, Yesu Kristo, ambaye angeteseka kulipia gharama na kutoa msamaha kwa dhambi zilizoungamwa. …
Mpango wa Baba yetu wa Mbinguni unatoa misaada mingine ili kutuongoza kupitia safari zetu za duniani. Nitazungumza juu ya minne kati ya hii. …
Kwanza, ninazungumza juu ya Nuru au Roho ya Kristo. Katika mafundisho yake makuu katika Kitabu cha Moroni, Moroni ananukuu mafundisho ya baba yake kwamba “Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili ajue mema na maovu” (Moroni 7:16). …
Msaada mwingine mkubwa wa pili unaotolewa na Bwana ili kutusaidia kuchagua kilicho chema ni kundi la maelekezo ya kiungu katika maandiko kama sehemu ya mpango wa wokovu (mpango wa furaha). Maelekezo haya ni amri, ibada na maagano.
Amri zinafafanua njia ambayo Baba yetu wa Mbinguni ameitoa kwa ajili yetu sisi ili tupige hatua kuelekea uzima wa milele. …
Ibada na maagano ni sehemu ya sheria ambayo inafafanua njia ya uzima wa milele. …
Misaada mingine iliyotolewa na Mungu kwa ajili ya kufanya chaguzi sahihi ni madhihirisho ya Roho Mtakatifu. …
Moja ya misaada muhimu zaidi ya Mungu kwa watoto Wake waaminifu ni kipawa cha Roho Mtakatifu. …
Kwa misaada mingi yenye nguvu ya kutuongoza katika safari za duniani, inakatisha tamaa kwamba wengi wanabaki bila kujiandaa kwa ajili ya wakati wao uliochaguliwa kukutana na Mwokozi na Mkombozi wetu, Yesu Kristo.
Unyenyekevu na tumaini katika Bwana ndizo tiba kwa michepuko hiyo.