Kikao cha Jumapili Asubuhi
Toba Yako Haimchoshi Yesu Kristo; Inaongeza Shangwe Yake
Dondoo
Leo ninataka kuzungumza na wale kati yetu ambao wakati mwingine mnahisi, “Toba na msamaha huonekana kufanya kazi kwa kila mtu isipokuwa mimi.”…
Nimejifunza kwamba ikiwa utangoja hadi uwe safi vya kutosha au mkamilifu vya kutosha ili kwenda kwa Mwokozi, utakuwa umeelewa vibaya! …
Ninashuhudia kwamba wakati Mungu anajali kuhusu makosa yetu, Yeye anajali zaidi kile kinachotokea baada ya kufanya makosa. Je, tutamgeukia tena na tena? …
Mwaliko wa kutubu ni dhihirisho la upendo wa Mungu.
Kusema ndiyo kwa mwaliko huo ni dhihirisho la upendo wetu. …
Hatubaki kwenye njia ya agano kwa kutofanya kosa kamwe. Tunabaki kwenye njia kwa kutubu kila siku.
Na wakati tunapotubu, Mungu anasamehe bila kutuaibisha, kutulinganisha na yeyote au kutugombeza kwa sababu hili ni jambo lilelile tulilokuwa tunalifanyia toba wiki iliyopita.
Anapendezwa kila mara Yeye anapotuona tukiwa magotini. Yeye anafurahia kutusamehe kwa sababu Kwake Yeye sisi tuna furaha!
Huhisi tu kwamba hiyo ni kweli?
Basi kwa nini ni vigumu sana kwetu kuamini?! Shetani, mshitaki mkuu na mdanganyifu, hutumia aibu kututenga mbali na Mungu. …
… Thamani yako daima ni “kubwa mbele ya Mungu,” bila kujali maamuzi yako yamekupeleka wapi. …
Ninasimama hapa kushuhudia kwamba Yesu Kristo hutoa nuru kwa wale wanaokaa gizani. … Tembea na uwashe Nuru—Mng’aro wetu Mkamilifu wa Tumaini.