Kikao cha Jumamosi Mchana
Maandalizi Binafsi Kukutana na Mwokozi
Dondoo
Wakati Rais Nelson anapozungumza kuhusu Ujio wa Pili, daima ni kwa matumaini mema ya shangwe. Hata hivyo, msichana wa Msingi hivi karibuni aliniambia kwamba yeye anakuwa na wasiwasi wakati wowote Ujio wa Pili unapotajwa. Alisema, “Ninakuwa na woga kwa sababu vitu vibaya vinatokea kabla Yesu hajaja tena.”
… Ushauri bora kwake, kwako, na kwangu ni kufuata mafundisho ya Mwokozi. …
Kuelekea mwisho wa huduma Yake ya duniani, Yesu Kristo aliulizwa ni lini Yeye angerudi tena. …
Mwokozi kwanza alisema fumbo la wanawali kumi. …
Somo muhimu la fumbo hili la wanawali kumi ni kwamba tunakuwa na hekima tunapokubali injili, kutafuta kuwa na Roho Mtakatifu kuwa pamoja nasi na kuepuka udanganyifu. … Tunapaswa kufanya hivi kwa ajili yetu wenyewe.
Mwokozi kisha alisema fumbo la talanta. …
Ujumbe mmoja wa fumbo ni kwamba Mungu anatutarajia sisi kutanua uwezo tuliopewa, lakini Yeye hataki sisi tulinganishe uwezo wetu na ule wa wengine. …
Mwishowe, Mwokozi alisema fumbo la kondoo na mbuzi. …
Somo la fumbo la Mwokozi la kondoo na mbuzi ni kwamba tunapaswa kutumia vipawa vyetu tulivyopewa—muda, talanta na baraka—kuwatumikia watoto wa Baba wa Mbinguni, hasa wale walio hatarini na wenye uhitaji.
Mwaliko wangu kwa yule mtoto wa Msingi mwenye wasiwasi niliyemtaja hapo awali, na kwa kila mmoja wenu, ni kumfuata Yesu Kristo na kumtumainia Roho Mtakatifu kama vile ambavyo ungefanya kwa rafiki wa thamani.