Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Mbele ya Macho Yetu
Dondoo
Tunashukuru kuwepo duniani wakati Kanisa linaongezeka kwa idadi na ushawishi, lakini muhimu zaidi katika mioyo na maisha ya waumini wake. …
Leo Kanisa lina mahekalu 367 katika hatua mbalimbali za usanifu, ujenzi, au uendeshaji. … Akina kaka na dada, tunaharakisha utakatifu wetu tunapokuwa wastahiki kuingia hekaluni, tunapoabudu katika nyumba ya Bwana, na tunapofanya maagano na Mungu kwa ajili yetu wenyewe na kwa niaba ya mababu zetu upande wa pili wa pazia. …
Tunaona Bwana akiharakisha kazi Yake katika misheni. … Zaidi ya idadi, roho ya kukusanyika ni kuleta nafsi kwa Yesu Kristo na injili Yake. …
Tunamwona Bwana akiharakisha fursa za elimu kwa waumini wetu na hata wale wasio wa imani yetu ulimwenguni kote. …
Hivi sasa zaidi ya wanafunzi 800,000 ulimwenguni kote wameandikishwa katika seminari na chuo, uandikishaji wa juu zaidi katika historia ya Kanisa. …
Eneo lingine ambalo linaonyesha kuongezeka kwa elimu katika Kanisa ni BYU-Pathway Worldwide. … Kukamilisha kozi kunamaanisha kupata ajira, na upatikanaji wa ajira unamaanisha maisha bora kwa familia na fursa zaidi za kumtumikia Bwana. …
Ninatambua kwamba katikati ya habari njema ya injili, kuna wale wanaosumbuka, ambao wana changamoto za imani, mashaka, na maswali ambayo yanaonekana hayana majibu. Akina kaka na dada, Yesu Kristo ndiye jibu. Anza na Yeye. Tafuta mkono Wake katika maisha yako. Msikilize Yeye. …
Jua kwamba Yeye anaelewa.