Mkutano Mkuu
Misaada ya Kiungu kwa ajili ya Maisha ya Duniani
Mkutano mkuu wa Aprili 2025


14:40

Misaada ya Kiungu kwa ajili ya Maisha ya Duniani

Mpango wa Baba yetu wa Mbinguni unatoa misaada ili kutuongoza kupitia safari zetu za duniani.

I.

Kupitia Nabii Joseph Smith, Bwana alifunua mambo machache kuhusu maisha yetu kabla ya kuzaliwa duniani. Huko, tulikuwepo kama watoto wa kiroho wa Mungu. Kwa sababu Mungu alitamani kuwasaidia watoto Wake wapige hatua, aliamua kuumba dunia ambapo tungepokea mwili, kujifunza kupitia uzoefu, kukuza sifa za kiungu na kujaribiwa kuona ikiwa tutatii amri za Mungu. Wale watakaostahili “watapata kuongezewa utukufu juu ya vichwa vyao kwa milele na milele” (Abraham 3:26).

Ili kuanzisha masharti ya mpango huu wa kiungu, Mungu alimchagua Mwanaye wa Pekee kuwa Mwokozi wetu. Lusiferi, ambaye mpango wake mbadala uliopendekezwa ungeharibu haki ya kujiamulia ya mwanadamu, akawa Shetani na “akatupwa chini.” Akifukuzwa kuja duniani na kunyimwa fursa ya maisha ya duniani, Shetani aliruhusiwa kuwajaribu “kuwadanganya na kuwapofusha watu, na kuwaongoza utumwani kadiri apendavyo, hata wengi kadiri wasivyosikia sauti ya [Mungu]” (Musa 4:4).

Muhimu kwenye mpango mkuu wa Mungu kwa ajili ya ukuaji wa watoto wake duniani ilikuwa ni kwa wao kupata uzoefu wa “upinzani katika vitu vyote” (2 Nefi 2:11). Kama vile ambavyo misuli ya mwili haiwezi kujengeka au kuendelezwa bila juhudi dhidi ya kani ya mvutano, kadhalika ukuaji wa duniani unamhitaji mwanadamu kuweka juhudi dhidi ya majaribu ya Shetani na mengine ya duniani. Muhimu zaidi kwa ukuaji wa kiroho ni hitaji la kuchagua kati ya jema na ovu. Wale wanaochagua mema watapiga hatua kuelekea hatma yao ya milele. Wale wanaochagua maovu—na sote tutafanya hivyo katika majaribu mbalimbali ya duniani—wangehitaji msaada wa kuokoa, ambao Mungu mwenye upendo aliuandaa kutupatia.

II.

Bila shaka, msaada wenye nguvu zaidi wa Mungu ulikuwa kumtoa Mwokozi, Yesu Kristo, ambaye angeteseka kulipia gharama na kutoa msamaha kwa dhambi zilizoungamwa. Dhabihu ile ya kulipia dhambi ya huruma na tukufu inafafanua kwa nini imani katika Bwana Yesu Kristo ni kanuni ya kwanza ya injili. Dhabihu Yake ya kulipia dhambi “huleta ufufuo wa wafu” (Alma 42:23) na “inalipia dhambi za ulimwengu” (Alma 34:8), ikifuta dhambi zetu zote tulizozitubu na kumpa Mwokozi wetu nguvu ya kutusaidia katika madhaifu yetu ya duniani.

Mwokozi Yesu Kristo

Zaidi ya ufutaji huo mtukufu wa dhambi zilizotendwa na kusamehewa, mpango wa Baba mwenye upendo wa Mbinguni hutoa zawadi zingine nyingi ili kutulinda, ikiwa ni pamoja na kutulinda kutokana na kufanya dhambi kwa mara ya kwanza. Maisha yetu ya duniani daima huanza na baba na mama. Kwa hakika, wote wapo, wakiwa na vipawa tofauti ili kuongoza ukuaji wetu. Ikiwa si hivyo, kutokuwepo kwao ni sehemu ya upinzani ambao lazima tuushinde.

III.

Mpango wa Baba yetu wa Mbinguni unatoa misaada mingine ili kutuongoza kupitia safari zetu za duniani. Nitazungumza juu ya minne kati ya hii. Tafadhali msinitake nitaje yote minne, kwa sababu misaada hii ina uhusiano. Zaidi, kuna ulinzi mwingine wa huruma katika kuongezea kwenye hii.

Kwanza, ninazungumza juu ya Nuru au Roho ya Kristo. Katika mafundisho yake makuu katika Kitabu cha Moroni, Moroni ananukuu mafundisho ya baba yake kwamba “Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili ajue mema na maovu” (Moroni 7:16). Tunasoma fundisho sawa na hili katika ufunuo wa siku za leo:

“Na Roho hutoa nuru kwa kila mtu ajaye katika ulimwengu; na Roho humwangazia kila mtu kote ulimwenguni, yule aisikilizaye sauti ya Roho” (Mafundisho na Maagano 84:46).

Tena: “Kwani Roho yangu imetolewa ulimwenguni kuwaangaza wanyenyekevu na waliopondeka, na kwa kuwahukumu wasio mcha Mungu” (Mafundisho na Maagano 136:33).

Rais Joseph Fielding Smith alifafanua maandiko haya: “Bwana hajawaacha wanadamu (wakati wanapozaliwa kwenye ulimwengu huu) bila usaidizi, wakipapasa kutafuta nuru na ukweli, bali kila mwanadamu … amezaliwa akiwa na haki ya kupokea mwongozo, maelekezo, ushauri wa Roho ya Kristo au Nuru ya Ukweli.”

Kujifunza Maandiko.

Msaada mwingine mkubwa wa pili unaotolewa na Bwana ili kutusaidia kuchagua kilicho chema ni kundi la maelekezo ya kiungu katika maandiko kama sehemu ya mpango wa wokovu (mpango wa furaha). Maelekezo haya ni amri, ibada na maagano.

Amri zinafafanua njia ambayo Baba yetu wa Mbinguni ameitoa kwa ajili yetu sisi ili tupige hatua kuelekea uzima wa milele. Watu wanaofikiria amri kama njia ya Mungu kuamua nani wa kumuadhibu wanashindwa kuelewa dhumuni hili la mpango wa furaha wa Mungu mwenye upendo. Kwenye njia hiyo, hatua kwa hatua tunafikia uhusiano unaohitajika na Mwokozi wetu na kustahili kwa ajili ya ongezeko la nguvu Yake kutusaidia katika njia yetu kuelekea hatma ambayo Yeye anaitamani kwa ajili yetu sote. Baba yetu wa Mbinguni anatamani watoto Wake wote warudi kwenye ufalme wa selestia, ambapo Mungu na Mwokozi wetu wanaishi na kuwa na aina ya maisha ya wale wanaoishi katika utukufu huo wa selestia.

Ibada na maagano ni sehemu ya sheria ambayo inafafanua njia ya uzima wa milele. Ibada na maagano matakatifu tunayofanya na Mungu kupitia kushiriki ibada hizo, ni hatua zinazohitajika na ulinzi muhimu kwenye njia hiyo. Ninapenda kufikiria jukumu la maagano kama mfano kwamba chini ya mpango wa Mungu, baraka Zake za juu zaidi hutolewa kwa wale wanaoahidi kabla, kutii amri fulani na wale wanaotii ahadi hizo.

Misaada mingine iliyotolewa na Mungu kwa ajili ya kufanya chaguzi sahihi ni madhihirisho ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni mshiriki wa tatu wa Uungu. Kazi yake, iliyofafanuliwa katika maandiko, ni kushuhudia juu ya Baba na Mwana, kutufundisha, kutukumbusha vitu vyote na kutuongoza kwenye ukweli wote. Maandiko yanajumuisha maelezo mengi ya madhihirisho ya Roho Mtakatifu, kama vile ushahidi wa kiroho katika kujibu ombi kuhusu ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Dhihirisho halipaswi kueleweka kama kipawa cha Roho Mtakatifu, ambacho hutolewa kufuatia ubatizo.

Moja ya misaada muhimu zaidi ya Mungu kwa watoto Wake waaminifu ni kipawa cha Roho Mtakatifu. Umuhimu wa kipawa hiki ni dhahiri katika ukweli kwamba kinatolewa rasmi baada ya toba na ubatizo kwa maji, “na kisha [maandiko yanafafanua] unakuja msamaha wa dhambi zenu kwa moto na kwa Roho Mtakatifu” (2 Nefi 31:17). Watu walio na msamaha huu wa dhambi—na kisha mara kwa mara kufanya upya utakaso kwa toba ya kila siku na kuishi kulingana na agano waliloweka kupitia ibada ya sakramenti—wanastahili ahadi kwamba Roho Mtakatifu, Roho ya Bwana, “awe pamoja nao … daima” (Mafundisho na Maagano 20:77).

Rais Joseph F. Smith

Basi, Rais Joesp F. Smith alifunza kwamba Roho Mtakatifu “ataangazia akili za watu kwa mambo yanayomhusu Mungu, kuwasadikisha wakati wa uongofu wao kuhusu utendaji wa mapenzi ya Baba na kuwa ndani yao ushuhuda wa kudumu kama mwenza katika maisha, akitenda kama mwongozo wa hakika na salama kwenye ukweli wote na kuwajaza siku hadi siku kwa shangwe na furaha, kwa tamanio la kutenda mema kwa wanadamu wote, kuteseka kwa ajili ya mabaya badala ya kufanya mabaya, kuwa wakarimu na wenye huruma, wenye uvumilivu na wenye hisani. Wote wenye kipawa hiki kisichokadirika, lulu hii ya thamani kuu, wana kiu endelevu ya haki. Bila usaidizi wa Roho Mtakatifu,” hakuna mwanadamu anayeweza kutembea kwenye njia nyembamba iliyonyooka.”

IV.

Kwa misaada mingi yenye nguvu ya kutuongoza katika safari za duniani, inakatisha tamaa kwamba wengi wanabaki bila kujiandaa kwa ajili ya wakati wao uliochaguliwa kukutana na Mwokozi na Mkombozi wetu, Yesu Kristo. Mfano wake wa wanawali kumi, uliozungumzawa sana katika mkutano huu, unapendekeza kwamba kati ya wale walioalikwa kukutana Naye, nusu yao pekee watakuwa hawakujiandaa.

Wanawali kumi.

Sote tunajua juu ya mifano ya watu ambao hawajajiandaa: wamisionari waliorudi ambao wamevuruga ukuaji wao wa kiroho kwa vipindi vya kutoshiriki kikamilifu, vijana ambao wamehatarisha ukuaji wao wa kiroho kwa kushindwa kushiriki katika mafundisho na shughuli za Kanisa, wanaume ambao wameghairi utawazo wao kwenye Ukuhani wa Melkizedeki, wanaume na wanawake—wakati mwingine uzao wa waanzilishi wenye heshima au wazazi wenye kustahili—ambao wameacha njia ya agano kabla ya kufanya na kushika maagano ndani ya hekalu takatifu.

Sala binafsi.

Michepuko mingi ya namna hiyo hutokea wakati waumini wanaposhindwa kufuata mpango wa marekebisho ya msingi ya kiroho wa sala binafsi, usomaji wa maandiko mara kwa mara na toba ya mara kwa mara. Kinyume, baadhi wanapuuza ufanyaji upya wa maagano kila wiki kwa kutopokea sakramenti. Baadhi wanasema Kanisa halikidhi mahitaji yao; wakibadilisha kile wanachokiona kama mahitaji yao ya baadaye kuwa juu ya kile ambacho Bwana amekitoa katika mafundisho Yake mengi na fursa kwa ajili ya huduma muhimu kwa wengine.

Unyenyekevu na tumaini katika Bwana ndizo tiba kwa michepuko hiyo. Kama vile Kitabu cha Mormoni kinavyofundisha, Bwana “huwabariki na kuwafanikisha wale ambao huweka imani yao kwake” (Helamani 12:1). Kumtumaini Bwana ni hitaji la kipekee kwa wote wanaopima kimakosa amri za Mungu na mafundisho ya manabii Wake dhidi ya matokeo ya hivi karibuni ya hekima ya mwanadamu.

Nimezungumza juu ya misaada mingi ya duniani ambayo Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo ameitoa ili kuwasaidia watoto Wake warudi Kwake. Sehemu yetu katika mpanngo huu wa kiungu ni kumtumaini Mungu na kutafuta na kutumia misaada hii ya kiungu, hasa Upatanisho wa Mwanawe Mpendwa, Mwokozi wetu, na Mkombozi wetu, Yesu Kristo. Ninasali kwamba tutafundisha na kuishi kanuni hizi, katika jina la Yesu Krist, amina.