Mkutano Mkuu
Imani: Mapatano ya Kuaminiana na Uaminifu
Mkutano mkuu wa Aprili 2025


11:17

Imani: Mapatano ya Kuaminiana na Uaminifu

Imani huchipuka wakati tunapomtumaini Yesu Kristo na huchanua wakati tunapokuwa waaminifu Kwake.

Nilipokuwa na umri wa miaka 17, nilifanya makubaliano na rafiki yangu José Luis kumfundisha jinsi ya kuogelea. Hivyo asubuhi moja tulitenga muda wa kufanya mazoezi. Wakati somo letu lilipomalizika na nilipokuwa nikitoka kwenye bwawa la kuogelea, nilimsikia rafiki yangu akipiga kelele kuomba msaada. Alikuwa akizama kwenye eneo lenye kina kirefu cha bwawa hilo la kuogelea.

Nilijirusha majini na kuogelea kuelekea aliko yeye huku nikisali kuomba msaada. Nilipoushika mkono wake kumvuta ili kumleta nje ya maji, rafiki yangu aliyekata tamaa alipanda mgongoni mwangu na kunishika kabari. Sasa wote tulikuwa tukizama. Nikijaribu kwa kadiri niwezavyo kutoka nje ya maji, nilisali kwa jitihada zangu zote kwa ajili ya muujiza kutoka kwa Mungu. Kisha, taratibu lakini kwa uthabiti nguvu ya Mungu ilijidhihirisha wakati nilipohisi mkono ukinisukuma kuelekea sehemu yenye kina kifupi cha bwawa la kuogelea, ukituleta kwenye usalama.

Uzoefu huu unathibitisha somo kuu ambalo Rais Russell M. Nelson aliwahi kulifundisha: “Unapotafuta nguvu za Bwana katika maisha yako kwa nguvu sawa na zile ambazo mtu anayezama anakuwa nazo wakati akitapatapa na kutafuta hewa, nguvu kutoka kwa Yesu Kristo zitakuwa zako.”

Watoto na vijana wapendwa, leo ninataka kuzungumza nanyi kuhusu kanuni muhimu ya imani katika Yesu Kristo.

Imani katika Kristo Humaanisha Kumwamini Yeye

Je, humaanisha nini kuwa na imani katika Kristo? Je, humaanisha kwamba tunamwamini Yeye au kuwa na ushuhuda kwamba kweli ni Yeye? Huo unaweza kuwa ni mwanzo, lakini ni zaidi ya hilo. Je umewahi kuifikiria imani kuwa kama kumwamini? Fikira kuhusu mtu ambaye unamwamini sana—pengine mwanafamilia au rafiki Je, ni kwa nini unawaamini? Inawezekana ni kwa sababu umehisi upendo na msaada thabiti.

Wakati tunapokuwa na imani katika Kristo, tunatambua baraka Zake na kukuza uhusiano wa kuaminiana na Yeye.

Je, Unawezaje Kuongeza Kuamini Kwako katika Kristo

Katika ibada ya hivi karibuni ya vijana, mlialikwa kutafakari juu ya wakati katika maisha yako ambapo ulipokea mwale wa mwangaza wa mbinguni. Jaribu zoezi hili!

Anza kwa kutafakari kuhusu Kristo na furaha ambayo huletwa maishani mwako na Upatanisho Wake na injili Yake. Pia, weka kumbukumbu ya “nyakati za kiroho” ambapo Mungu amekuwa pale kwa ajili yako, kwa ajili ya wapendwa wako na watu katika maandiko matakatifu. Sasa, shuhuda hizi hazitaleta nguvu maishani mwako mpaka Roho atakapozichora kwenye “mbao za nyama” za moyo wako. Kwa hiyo tafakari na weka kumbukumbu ya yote ambayo Mungu ameyaweka katika mwendo kwa ajili ya miujiza hii kuja tu kwa wakati sahihi.

Kisha, tumia zoezi hili kama fursa ya kusonga karibu zaidi na Mungu. Sali kwa Baba yako wa Mbinguni kama vile ilikuwa ndio mara ya kwanza. Elezea upendo na shukrani kwa sababu ya baraka Zake. Hata muulize Yeye namna Yeye anavyojisikia kuhusu wewe na kuhusu mwelekeo wa maisha yako.

Kama ukiwa mwaminifu na mnyenyekevu, utasikia jibu Lake na kuanza uhusiano binafsi na wa kudumu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Si hivyo tu, lakini pia tabia zako za kidini zitakuwa zenye maana. Kwa mfano, utatazamia sala zako, kujifunza binafsi na kuabudu hekaluni kama fursa za kupata kuwajua Wao na kuwa pamoja Nao.

Imani Inastawi kwa Uaminifu

Tambua kwamba imani huchipuka wakati tunapomwamini Yesu Kristo na huchanua wakati tunapokuwa waaminifu Kwake. Kama unataka uhusiano wa kweli na Kristo, muonyeshe Yeye kwa kufanya maagano na kuyashika kwa uaminifu na ukweli. Kufanya maagano na Yesu Kristo hujenga tumaini. Kuyaheshimu kunajenga imani.

Acha nitumie mfano binafsi: Wakati nilipokuwa mtoto, siku moja nilimkuta mama yangu akilia pekee yake. Niilipomuuliza kwa nini, alisema kwa upole, “ninahitaji uwe mvulana mwema.” Japokuwa nilijua kwamba sikuwa chanzo cha majonzi yake, nilimpenda na kumuamini mama yangu kuliko mtu mwingine ye yote na nilitaka kufanya maisha yake kuwa mepesi. Hivyo, nikiwa na machozi machoni mwangu na nikiwa na dhamiri ya dhati ya kijana wa miaka tisa, nilimuahidi siku hiyo kwamba daima ningejitahidi kuwa kijana mwema na kumfanya ajivunie.

Unaweza kufikiria nguvu ambayo ahadi hiyo ilikuwa nayo—na bado inayo—kwangu mimi?

Ahadi hiyo kwake ingeongoza maisha yangu. Kabla ya kufanya maamuzi, ningefikiria kama matendo yangu yangemfurahisha. Mapatano ya ahadi hii na uhusiano na mama yangu vilikuwa nanga kwa ajili ya mwenendo wangu maisha yangu yote.

Miaka mingi baadaye, wakati nilipokuja kumjua Yesu Kristo vyema zaidi, nilikuwa tayari nikijua namna ya kuweka imani yangu Kwake. Niliweka maagano na Bwana, na kadiri nilivyotafuta kuyaheshimu, amesamehe dhambi zangu, ameongoza maisha yangu na “kunijaza upendo Wake” kwa kina nafsini mwangu. Kristo alianzisha kwangu upendo wa kina, heshima, na uaminifu Kwake.

Je, mnaelewa kwa nini “imani ni kanuni ya matendo” na kwamba “pasipo imani haiwezekani kumpendeza [Mungu]”?

Wakati unapojaribu kufanya kinachompemdeza Yeye, utasema kama Yusufu wa Misri wakati alipojaribiwa na mke wa Potifa, “Ninawezaje basi kutenda uovu huu mkuu na nimkosee Mungu?” Na unapokumbana na upinzani, utasema kama kijana Nabii Joseph, “Nilijua hivyo, nami nilijua kwamba Mungu alijua, na sikuweza kukataa: …nilijua kwamba kwa kufanya hivyo ningemuudhi Mungu.”

Basi imani katika Yesu Kristo ni mapatano ya kuaminiana yanayojengwa katika uaminifu na upendo. Kwa maneno mengine, kuwa na shukrani kwa sababu ya upendo wa Mungu wenye rehema (hesed), tunaonyesha upendo wetu wa uaminifu (emunah) kwa kutii amri Zake.

Kristo anaahidi, “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika … atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhirihisha kwake.” Kama utaweka nia ya dhati ya kuwa mwaminifu Kwake, Yeye atadhihirisha upendo Wake kwa ajili yako

Imani kwenye Kukabiliana na Dhiki

Lakini ni kwa namna ipi tunapaswa kuitikia hali hiyo ya kujaribiwa ambayo inahitaji miujiza Yake? Wakati changamoto haziepukiki na wakati mwingine zinaogopesha, kiurahisi tembea pasipo shaka kuelekea Kwake, kama dhima ya KNV ya 2025 inavyoalika: “Nitegemeeni katika kila wazo; msitie shaka, msiogope.”

Unawezaje Kutembea Pasi na Shaka Kuelekea Kwake?

Fikiria kwamba wewe ni mchunguzi kwenye himaya usio ijua. Ili kushinda vikwazo mbele yako, unahitaji chanzo cha mwanga. Uaminifu wako kwa Mungu na mwingiliano wako endelevu na Yeye ni mafuta kwa ajili ya taa yako. Hivyo wakati unapokutana na giza na nyakati za kuogofya, badala ya kutembea kuzielekea bila kuwa na uoni, utawasha taa yako iliyojaa mafuta ya imani katika Kristo ili kumwaga mwanga wa matumaini angavu kwenye njia isiyo na uhakika. Uzoefu wako wa awali utaongeza tumaini lako kwamba Bwana atakusaidia kwenye safari yako.

Msafiri akiwa na taa ya mafuta.

Ni kwa Muda Gani Utaendelea na Tumaini na Imani katika Kristo?

Mnakumbuka hadithi yangu ya kwenye bwawa la kuogelea? Katika wakati huo wa kukata tamaa, muujiza ulikuja katika njia niliyoitegemea, lakini Mungu hatoi hakikisho kwamba mara zote itakuwa kulingana na mapenzi yetu. Imani yetu lazima ijikite katika Kristo na tumaini letu katika baraka Zake, kwa kadiri anavyoamua kuzitoa. “Tazamieni miujiza,” lakini “mwacheni Mungu ashinde katika maisha yetu.”

Ahadi za Mungu kwa Watu Wake Waaminifu

Marafiki zangu wadogo, ni kwa kiasi gani tunawaamini na kuwapenda! Ninyi ni sehemu ya familia ya Mungu na ni watoto wa agano. Sadiki na amini katika Yesu Kristo. Yeye atawawezesha ninyi kuwa wanafunzi Wake wa kweli.

Ninawaalika kuanzia leo kulea uhusiano wenu na Yesu Kristo. Weka ahadi ya kamwe kutomuacha Yeye.

Uaminifu wenu, upendo, kumwamini Kristo vitatengeneza sifa yenu na utambulisho kama ule wa Kwake. Mtapata ujasiri na nguvu za kushinda mashambulizi ya Shetani. Na wakati mnapofanya makosa, mtatamani msamaha Wake. Hatimaye, tumaini lenu kwa ajili ya siku za mbeleni litakuwa angavu. Yeye atawaamini kwa kuwapa nguvu Zake kukamilisha kitu cho chote Anachotegemea mkikamilishe, hata nguvu za kurudi kwenye uwepo Wake.

Ninawashuhudia juu ya shangwe ambayo huja kutokana na kuimba “wimbo wa upendo wa ukombozi” na “kuzungukwa milele na mikono yenye upendo wake.” Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Kuvuta Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2017, 42.

  2. Neno imani hutokana na fides, la Kilatini, ambalo humaanisha “kutumainia” (ona Michiel de Vaan, Etymological Dictionary of Latin and the other Italic languages (2008), under “fido.” The Greek cognate, πίστις, translates as “trusting” (see Robert Beekes, Etymological Dictionary of Greek [2010], 1:1161–62).

  3. “Imani ni kuwa na ujasiri na kutumaini katika Yesu Kristo” (Mwongozo wa Maandiko, “Imani,” Maktaba ya Injili).

  4. Ona “Look Unto Christ” (worldwide discussion for youth, Jan. 5, 2025), Maktaba ya Injili; ona pia Alexander Dushku, “Nguzo na Miale,” Liahona, Mei 2024, 14–16.

  5. Ona Neil L. Andersen, “Kumbukumbu za Kuelekeza Kiroho,” Liahona,, Mei 2020, 18–22.

  6. Ona 2 Wakorintho 3:2–3; ona pia Moroni 10:3; Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 88–92.

  7. Ona Ronald A. Rasband, “Kwa Mpango Mtakatifu,” Liahona, Nov. 2017, 55–57.

  8. Ona Mosia 2:20-21; Mafundisho na Maagano 59:21.

  9. Ona “Appendix 1: Sixth Theological Lecture on Faith, circa January–May 1835, as Published in Latter Day Saints’ Messenger and Advocate,” 124–25, josephsmithpapers.org.

  10. Ona Moroni 7:41; ona pia Stephen M. Covey and Rebeccz R. Merrill, The Speed of Trust: The One Thing that Changes Everything (2006), 215.

  11. 2 Nefi 4:21.

  12. “Mungu ni rafiki yangu. Katika yeye nitapata faraja. … Natamani kuwa pamoja na Kristo. Sihesabu maisha yangu kuwa ya thamani [isipokuwa] kutenda mapenzi yake.” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 243–44).

  13. Bible Dictionary, “Faith.”

  14. Waebrania 11:6.

  15. Ona Yohana 8:29.

  16. Mwanzo 39:9.

  17. Joseph Smith—Historia ya 1:25.

  18. Rais Gordon B. Hinckley alifundisha, “Kusali kwa Baba yako wa Mbinguni katika jina la Bwana Yesu Kristo, na mara zote, katika hali zote, kwa uhalisia wa maisha yako onyesha uaminifu na upendo wako.” (“Uaminifu,” Liahona, Mei 2003, 60; ona pia Brent J. Schmidt, Relational Faith: The Transformation and Restoration of Pistis as Knowledge, Trust, Confidence, and Covenantal Faithfulness [2022], 9; Teresa Morgan, Roman Faith and Christian Faith: Pistis and Fides in the Early Roman Empire and Early Churches [2015], 127–28).

  19. Ona Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022, 4–11.

  20. “Neno la kiebrania linalowakilisha imani ni אמונה (emunah) na ni neno linalojikita kwenye tendo likimaanisha ‘msaada.’ … Linaweka kitendo kwa yule ambaye ‘anamsaidia Mungu.’ Si mpaka kujua kwamba Mungu atatenda, lakini ni kwamba nitafanya ninachoweza kumsaidia Mungu. Wazo hili la kuusaidia ulimwengu emunah linaweza kuonekana kwenye Kutoka 17:12. … Ni msaada/emunah wa Haruni na Huri ambao uliibeba mikono ya Musa, na si msaada/emunah wa Musa. Tunaposema, ‘nina imani katika Mungu,’ tunapaswa kutafakari, ‘Nitafanya ninachoweza ili kumsaidia Mungu” (Jeff A. Benner, “Faith,” Ancient Hebrew Research Center, ancient-hebrew.org).

  21. Yohana 14:21; ona pia mstari wa 23.

  22. Ona Yohana 15:9–10.

  23. Ona Russell M, Nelson, “Kuvuta Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu,” 40–42.

  24. Mafundisho na Maagano 6:36.

  25. Neil L. Andersen, “Imani Si Bahati Nasibu Bali ni Chaguo,” Liahona, Nov. 2015, 65–68.

  26. Russell M. Nelson, “Nguvu ya Kasi ya Kiroho,” Liahona, Mei 2022, 99.

  27. Ona Russell M. Nelson, “Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 92–95.

  28. Ona Russell M. Nelson, “Children of the Covenant,” Ensign, May 1995, 32:

  29. Jesus is my friend. None other has given me so much. … Ninatumaini kwamba nitaonekana mwenye kustahili kuwa rafiki Yake” (Gordon B. Hinckley, “My Testimony,” Liahona, Julai 2000, 85).

  30. Ona Yohana 6:67–68; Mafundisho na Maagano 6:20.

  31. Ona Russell M. Nelson, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, May 15, 2022), Gospel Library; Richard G. Scott, 21 Principles: Divine Truths to Help You Live by the Spirit (2013), 90.

  32. Ona Alma 48:17.

  33. Ona Mosia 4:2; Moroni 36:18.

  34. Ona Thomas S. Monson, “Jipe Moyo,” Liahona, May 2009, 92.

  35. Ona Isaya 58:9; Helamani 10:4–5; Etheri 12:30; Moroni 7:33.

  36. Ona 2 Nefi 25:23.

  37. Alma 5:26; ona pia Alma 5:9; 26:13.

  38. 2 Nefi 1:15.