Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Aprili 2025


8:23

Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, sasa nitawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kuwaunga mkono kwako katika njia ya kawaida. Kama kuna wale wanaopinga mapendekezo yoyote, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono waonyeshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Jeffrey R. Holland kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, Ulisses Soares na Patrick Kearon.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka Sabini wafuatao watapumzishwa kutoka kwenye majukumu yao na kupewa hadhi ya heshima, kuanzia tarehe 1 Agosti 2025: Wazee David S. Baxter, Randall K. Bennett, Kevin S. Hamilton, Rafael E. Pino, na Jorge F. Zeballos.

Wale ambao wangependa kuonyesha shukrani kwa Ndugu hawa na kwa wake zao na familia zao kwa miaka mingi ya kujitolea katika utumishi Kanisani kote wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.

Pia tunampumzisha Mzee José A. Teixeira kutoka kwenye kuhudumu kama mshiriki wa Urais wa Sabini kuanzia tarehe Agosti 1, 2025.

Wale wanaopenda kuonyesha shukrani kwa Mzee Teixeira kwa huduma yake katika nafasi hii, tafadhali onyesheni.

Tunatambua kwa shukrani Sabini wa Maeneo 65 ambao watamaliza huduma yao na ambao majina yao yanaweza kupatikana katika tovuti ya Kanisa.

Wale wanaopenda kuungana pamoja nasi katika kuonyesha shukrani kwa ndugu hawa kwa huduma yao isiyo ya ubinafsi wanaweza kuonyesha.

Tunaupumzisha Urais Mkuu wa Wavulana ifikapo Agosti 1, 2025, kama ifuatavyo: Steven J, Lund kama Rais, Bradley R. Wilcox kama Mshauri wa Kwanza na Michael T. Nelson kama Mshauri wa Pili.

Wale wote wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa akina kaka hawa kwa huduma yao ya dhati, tafadhali waonyeshe.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Mzee Kelvin R. Duncan kama mshiriki wa Urais wa Sabini kuanzia Agosti 1, 2025.

Wale wanaounga mkono waonyeshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini Wakuu wapya wenye Mamlaka: John D. Amos, Ronald M. Barcellos, Steven C. Barlow, Kevin G. Brown, B. Corey Cuvelier, Michael Cziesla, James E. Evanson, Brik V. Eyre, Ozani Farias, Aaron T. Hall, Brian J. Holmes, Pedro X. Larreal, Clement M. Matswagothata, Eduardo F. Ortega, Edward B. Rowe na Wan-Liang Wu.

Wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunawapeni taarifa kwamba Sabini wa Maeneo wapya 78 walikubaliwa wakati wa mikutano ya mkutano mkuu wa uongozi iliyofanyika siku ya Alhamisi, Aprili 3, na baadaye kutangazwa kwenye tovuti ya Kanisa. Tunawaalikeni muwakubali ndugu hawa katika majukumu yao mapya.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Urais Mkuu mpya wa Wavulana, utakaoanza kazi ifikapo Agosti 1, 2025: Timothy L. Fames kama Rais, David J. Wunderli kama Mshauri wa Kwanza na Sean R. Dixon kama Mshauri wa Pili.

Wale wanaounga mkono waonyeshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha vivyo hivyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wanaounga mkono, tafadhali onyesheni kwa kuinua mkono.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada, kwa kura yenu ya kuwakubali kwa niaba ya uongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Maeneo

Sabini wa Maeneo wafuatao walikubaliwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Emmanuel Rodantes G. Abraham, Jonah Akekere, Edmund L. Ang, Odilon Asevedo, Vladimir N. Astashov, Douglas W. Atwood, Ignatius K. Baidoo, Anthony John Balledos, Carlos A. Baptista, Timothy L. Barney, Marco A. Becegato, Steven L. Bodhaine, Thaddeus M. Brown, Gabriel A. Campos, Jose R. Cardenas Vanegas, Palmênio C. Castro, Robert M. Chaggares, David L. Chandler, Andrew J. Child, Carlton J. Christensen, William G. Coleman, Sean F. D. Collins, Bryan C. Crawley, Gustavo A. Cristales, Loren G. Dalton, M. Sidney Daniels, Robert L. Davis, Freeman Dickie, Moroni Dominguez Jimenez, Siale Matavaha ‘Eliesa, Robert K Ellis, James G. Fantone, Jacob C. Fish, Matthias A. Frost, W. Brett Graham, Jeremy B. Grisel, Rodney H. Hillam, Shane T. Holdaway, James A. Jarvis, Aaron R. Jenne, Jose A. Jimenez Alava, Nathan L. Johnson, H. Jason Joseph, Ronald M. Judd, Motoshige Karino, Natthapol Lattisophonkul, Roland E. Léporé, Samuel López, Ricard G. Manáhan, Arturo Martinez, Charles P. Martins, Kelend I. Mills, David E. Mouhsen, Luis Navarro, Mathias N. Niambe, Jeffery M. Nikoia, Prince S. Nyanforh, Kabemba F. Nyembo, Akingbade A. Ojo, G. Michael Ortiz, Huri Parata, Juan C. Quilantan, David A. Reyes, Matthew O. Richardson, Matthew L. Riggs, Jaime N. Rivera Jr., Stephen M. Sargent, David L. Smith, Todd B. Smith, Marco N. Sosa, Jared M. Spataro, Scott Spencer, Craig M. Teuscher, Mees Bulang-C. Tshiband, Francisco Valim, Jesus A. Vazquez Roman, Terry E. Welch, David A. Winters.

Sabini wa Maeneo wafuatao watapumzishwa mnamo au kabla ya Agosti 1, 2025:

John D. Amos, Jay D. Andersen, Faapito Auapaau, Frederick K. Balli, Steven C. Barlow, Kevin W. Birch, John W. Boswell, Kevin G. Brown, J. Francisco Bührer, Suchat Chaichana, Christian C. Chigbundu, Matthew R. Clarke, L. Guido Cristobal, B. Corey Cuvelier, Edmarc R. Dumas, Brik V. Eyre, Timothy L. Farnes, Carlos A. Gabaldón, M. Andrew Galt, Vladislav Y. Gornostaev, Aaron T. Hall, Thomas Hänni, Richard I. Heaton, Broc C. Hiatt, Brian J. Holmes, David H. Huntsman, Norman Insong, Daniel Kabason, Federico M. Kähnlein, Jeffrey J. Kerr, David G. LaFrance, Marcelo Louza, Jose G. Manarin, Jeremiah J. Morgan, Mark A. Mortensen, S. Ephraim Msane, R. Pepper Murray, Eduardo F. Ortega, Nathan D. Pace, Michael M. Packer, Jorge W. Pérez, Kyrylo Pokhylko, Sergio A. Poncio, Art Rascon, Miguel A. Reynoso, Gustavo G. Rezende, Robert G. Rivarola, Edward B. Rowe, Alexey V. Samaykin, Luciano Sankari, Henry Savstrom, J. Matthew Scott, James E. Slaughter, Robert T. Smith, Ricardo Spencer, Colin C. Stauffer, David C. Stewart, Konstantin Tolomeev, Arlen M. Tumaliuan, Martin J. Turvey, Yan Carlos Vega, Paul B. Whippy, Chad R. Wilkinson, Dow R. Wilson, Markus Zarse.

Muhtasari

  1. Sabini hawa Wakuu wenye Mamlaka watakuwa na umri wa miaka 70 mwaka huu. Kama ilivyo desturi, watapumzishwa kutokana na majukumu yao na kupewa hadhi ya heshima, kuanzia tarehe 1 Agosti 2023.