Mkutano Mkuu
Mamlaka ya Kiungu, Wavulana Adhimu
Mkutano mkuu wa Aprili 2025


11:44

Mamlaka ya Kiungu, Wavulana Adhimu

Ni ushuhuda wangu kwamba wenye Ukuhani wa Haruni, pamoja na nguvu zake, ibada, na wajibu, hutubariki sisi sote.

Asante, Mzee Andersen, kwa maelezo ya kupendeza kuhusu nguvu ya ukuhani na juu ya nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi.

Januari hii, nilipokuwa nimeketi katika mkutano wa sakramenti, zaidi ya wavulana dezeni moja walikubaliwa kupandishwa katika Ukuhani wa Haruni. Nilihisi ulimwengu ukibadilika chini ya miguu yangu.

Ilinishangaza kwamba kote ulimwenguni, kulingana na saa za nchi husika, katika mikutano ya sakramenti kama ule, makumi elfu ya mashemasi, walimu na makuhani walikuwa wakikubaliwa ili kutawazwa kwenye huduma za ukuhani za maisha yote ambazo zingetanuka kwa urefu na upana kwenye ukusanyaji wa Israeli.

Kila Januari, mikono huwekwa juu ya vichwa vya wavulana takribani 100,000, ikiwaunganisha kupitia ibada kwenye mstari ulionyooka wa mamlaka unaorudi nyuma kupitia enzi za Urejesho kwa Joseph na Oliver, na Yohana Mbatizaji hadi kwa Yesu Kristo.

Letu daima siyo kanisa la maonyesho sana. Hapa, tunafanya urahisishaji.

Lakini bado, kuona makundi haya ya wenye ukuhani wapya waliotawazwa wakitembea kwa kishindo kama radi kote ulimwenguni, nilijiuliza—katika “kanisa la shangwe” kwa namna ya shangwe” kama haipaswi kutangazwa kutokea juu ya dari. “Leo,” niliwaza, “kunapaswa kuwe na matarumbeta na sauti ya juu na mishumaa ya Kirumi inayowaka sana. Kunapaswa kuwa na gwaride!”

Tukizijua nguvu za Mungu kwa hakika zilivyo, sisi tulikuwa mashahidi wa uvurugaji wa hasa mipangilio ya ulimwengu huu kwa mamlaka ya kiungu yakifurika duniani.

Utawazo huu unawaingiza wavulana hawa kwenye huduma ya maisha yote kadiri watakavyojikuta wenyewe katika nyakati zenye matokeo na sehemu ambapo uwepo wao na sala zao na nguvu za ukuhani wa Mungu walio nao vitakuwa na umuhimu.

Huu mnyororo ulio dhibitiwa wa mabadiliko ulianza na malaika mtumishi aliyetumwa na Mungu. Yohana Mbatizaji wa nyakati za kale aliyefufuka aliwatokea Joseph na Oliver, akaweka mikono yake juu ya vichwa vyao na kusema, “Juu yenu ninyi watumishi wenzangu, katika jina la Masiya, ninawatunukia Ukuhani wa Haruni, ambao hushikilia funguo za huduma ya malaika, na za injili ya toba, na za ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi” (Mafundisho na Maagano 13:1).

Yohana aliyaita mamlaka haya “Ukuhani wa Haruni,” kwa jina la kaka wa Musa na mwenza katika ukuhani. Hapo kale, wenye ukuhani wa Haruni huu walipaswa kufundisha na kusaidia katika ibada—ibada ambazo zilifokasi uanafunzi kwa Masiya wa siku zijazo, Bwana Yesu Kristo (ona Kumbukumba la Torati 33:10).

Kitabu cha Hesabu kwa uwazi kinatoa kwa wenye ukuhani wa Haruni majukumu ya kubeba vyombo vya ibada. “Nawe utawaweka Haruni na wanawe … na vitu watakavyovitunza … meza … na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika kutumika kwao.” (Hesabu 3:10, 31).

Ibada ya Agano la Kale la dhabihu ya mnyama ilitimilika na kupatiwa mbadala kupitia maisha na Upatanisho wa Mwokozi. Ibada hiyo ya kale ilibadilishwa kwa ibada sasa tunayoiita sakramenti ya Meza ya Bwana.

Bwana anawakabidhi leo wenye ukuhani wa Haruni wa siku za leo kufanya mambo yale yale waliyoyafanya hapo kale: kufundisha na kuhudumu katika ibada—yote kutukumbusha juu ya Upatanisho Wake.

Wakati mashemasi, walimu na makuhani wanaposaidia kwenye sakramenti, wanapokea baraka za sakramenti kama vile mwingine yeyote: kwa kushika agano wanalolifanya pale wao binafsi wanapopokea mkate na maji. Lakini katika utekelezaji wa majukumu haya matakatifu, wanajifunza pia zaidi kuhusu wajibu wao wa ukuhani.

Ukuhani wa Haruni unaitwa ukuhani wa maandalizi kwa sehemukwa sababu ibada zake uwaruhusu wao kupata uzoefu wa uzito na shangwe ya kuwa kwenye kazi ya Bwana, kuwaandaa wao kwa ajili ya huduma ya baadaye ya ukuhani, wakati wanapoweza kuitwa kuhudumu katika njia zisizotarajiwa—ikijumuisha kutamka baraka zenye mwongozo wa kiungu katika nyakati ambapo tumaini na ndoto na hata maisha na kifo, vikiwa havitabiriki.

Matarajio hayo makini yanahitaji maandalizi makini.

Mafundisho na Maagano inafafanua kwamba mashemasi na walimu wanapaswa “kuonya, kuelezea, kushawishi, na kufundisha, na kuwaalika wote kuja kwa Kristo,” (Mafundisho na Maagano 20:59). Kama nyongeza kwenye fursa hizi makuhani wanapaswa “kuhubiri … na kubatiza” (Mafundisho na Maagano 20:50).

Yote hayo yanaonekana kama mengi, lakini katika ulimwengu halisi, mambo haya yanatokea kiasili, na kote ulimwenguni.

Askofu mmoja aliwafundisha urais mpya wa akidi ya mashemasi yake wajibu huu. Kwa hiyo urais wa vijana ulianza kuzungumza kuhusu vile ambavyo hilo lingeonekana katika akidi na kata yao. Waliamua kwamba walipaswa kuanza kuwatembelea waumini wazee katika kata ili kuona kile walichohitaji na kisha kukifanya.

Kati ya wale walio wahudumia alikuwepo Alan, jirani ambaye hakuwa nadhifu, mara nyingi akitumia lugha chafu na wakati mwingine mwenye chuki. Wanda, mke wa Alan, alikuwa muumini wa Kanisa, lakini Alan alikuwa, kama tunavyosema, kazi kweli.

Lakini bado, mashemasi walifanya kazi, kwa ucheshi wakipuuza matusi yake, wakati wakiondoa theluji na kuondoa taka. Ni vigumu kuwachukia mashemasi, na Alan hatimaye alianza kuwapenda wao. Wakati fulani walimwalika kanisani.

“Sipendi kanisa,” alisema.

“Unatupenda,” walisema. “Basi, njoo pamoja nasi. Unaweza kuja tu kwenye mikutano yetu ya akidi kama unataka.”

Na kwa idhini ya askofu, alikuja—na aliendelea kuja.

Mashemashi wakawa walimu na kadiri walivyoendelea kumhudumia, aliwafundisha kufanya kazi kwenye magari na kujenga vitu. Wakati mashemasi hawa walipandishwa kuwa walimu na kuwa makuhani, Alan alikuwa akiwaita “wavulana wangu.”

Walikuwa sasa wakijiandaa kwa ajili ya kutumikia misheni na walimuomba kama wangeweza kufanya mazoezi ya masomo ya umisionari na yeye. Aliapa kwamba kamwe asingesikiliza au kuamini, lakini, wangeweza kufanya mazoezi nyumbani kwake.

Kisha Alan aliugua. Na alikuwa mnyeyekevu.

Siku moja, katika mkutano wa akidi, kwa upole aliwaomba wasali kwa ajili yake ili aache kuvuta sigara, walifanya hivyo. Lakini kisha walimfuata hadi kwake na kuondoa vyombo vyake vyote vya kutunzia tumbaku.

Wakati afya yake iliyozorota ilipomfanya Alan alazwe hospitali na kwenye vituo vya urekebishaji, “wavulana wake” walimhudumia, kimya kimya wakionesha nguvu za ukuhani na za upendo usio shindwa (ona Mafundisho na Maagano 121:41).

Muujiza uliendelea wakati Alan alipoomba kubatizwa—lakini kisha akafariki kabla ya hilo kutokea. Kama ombi lake, mashemasi wake waliokuwa sasa makuhani wakawa wasindikiza jeneza na wazungumzaji kwenye mazishi, ambapo—kwa usahihi—walionya, walielezea, walishawishi, walifundisha na kuwakaribisha watu wote kuja kwa Kristo.

Na baadaye, ndani ya hekalu, ilikuwa mmoja wa “wavulana wa Alan” aliyembatiza rais yule wa zamani wa akidi ya mashemasi kwa niaba ya Alan.

Kila kitu Yohana Mbatizaji alichosema kifanywe, walikifanya. Walifanya kile mashemasi, walimu, na makuhani hufkianya kote katika Kanisa hili na kote ulimwenguni.

Mojawapo ya vitu wenye ukuhani wa Haruni wamepatiwa jukumu juu yake hujumisha ibada ya sakramenti.

Mwaka uliopita, nilikutana na askofu mwenye mwongozo wa kiungu na mkewe wake wa ajabu. Kwenye safari ya hivi karibuni ya Jumamosi asubuhi, walikuwa wakielekea kwenye ubatizo wa mwana wao na walipata ajali iliyopelekea kifo cha Tess, binti yao mpendwa wa miaka miwili.

Asubuhi iliyofuata, waumini wa kata yao walikusanyika kwa ajili ya mkutano wa sakramenti wakiwa wamejaa huruma, pia wakiumia juu ya kumpoteza binti huyu mdogo mkamilifu. Hakuna aliyetarajia familia ya askofu kuwa kanisani asubuhi hiyo, lakini dakika chache kabla ya mkutano kuanza, familia ya askofu iliingia kwa utulivu.

Askofu alienda kwenye jukwaa na akakipita kiti chake cha siku zote katikati ya washauri wake na badala yake akaketi na makuhani wake kwenye meza ya sakramenti.

Katika usiku ule wenye maumivu na usio na usingizi kutafuta uelewa na amani, alikuwa amepokea msukumo wa kile familia yake ilichokihitaji zaidi—na kile kata yake ilichokihitaji zaidi. Kilikuwa ni kusikia sauti ya askofu wao, Rais wao wa Ukuhani wa Haruni kwenye kata, baba yao mwenye huzuni, akitamka ahadi za agano la sakramenti.

Hivyo, baada ya muda, alipiga magoti pamoja na makuhani wale na kuzungumza na Baba Yake. Kwa huzuni ya tukio lile, alitamka baadhi ya maneno yenye nguvu zaidi ambayo mtu yeyote amewahi kuruhusiwa kuyasema kwa sauti katika maisha haya.

Maneno yenye matokeo ya milele.

Maneno ya ibada.

Maneno ya agano.

Maelekezo ambayo yanatuunganisha na lengo hasa la maisha haya—na kwenye matokeo ya kupendeza zaidi ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu.

Je, unaweza kufikiria kile mkusanyiko ulichokisikia ndani ya nyumba ile ya mkutano—Walichokihisi kwenye maneno ambayo tunayasikia kila Jumapili kwenye nyumba zetu za mikutano?

“Ee, Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase mkate huu kwa roho za wale wote watakaoula, ili waweze kuula kwa ukumbusho wa mwili wa Mwanao, na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba wako radhi kujichukulia juu yao jina la Mwanao, na daima kumkumbuka, na kushika amri zake ambazo amewapa, ili daima Roho wake apate kuwa pamoja nao. Amina” (Mafundisho na Maagano 20:77).

Na kisha: “Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase [maji] haya kwa roho za wale wote watakaoyanywa, ili waweze kufanya hivi kwa ukumbusho wa damu ya Mwanao, ambayo ilimwagwa kwa ajili yao; kwamba washuhudie kwako, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba daima wamkumbuke, ili Roho wake apate kuwa pamoja nao. Amina” (Mafundisho na Maagano 20:79).

Baba huyu na mama huyu wema wanashuhudia kwamba ahadi hiyo imetimizwa. Wanapata, hakika, kwenye faraja yao ya milele, “kuwa na Roho wake pamoja nao.”

Nina shukrani milele kwamba wenye Ukuhani wa Haruni, pamoja na nguvu zake, ibada na wajibu, wanatubariki sote kupitia funguo za “huduma za malaika, na za injili ya toba, na za ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi” (Mafundisho na Maagano 13:1). Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Patrick Kearon, “Karibu katika Kanisa la Shangwe,” Liahona, Nov. 2024, 36–38.

  2. Kwenye ujumbe wake wa mkutano mkuu “Karibu Kwenye Kanisa la Shangwe,” Mzee Kearon alituelekeza kwenye tanbihi 10 ya mafundisho ya Rais Gordon B. Hinckley: “Wakati wewe, kama kuhani, unapopiga magoti wakati wa sakramenti na kutoa sala, ambayo ilikuja kupitia ufunuo, unawaweka wahudhuriaji wote kwenye agano na Bwana. Je, hili ni jambo dogo? Ni jambo muhimu na lisilo na kifani.( “The Aaronic Priesthood—a Gift from God,” Ensign, Mei 1988, 46.