Liahona
Wakati Mwili na Roho Vinapoungana
Januari 2026 Liahona


Sauti za Wanachama

Wakati Mwili na Roho Vinapoungana

Mnamo Julai 12, 2025, Kanisa lilikuwa mwenyeji wa tukio la kukumbukwa lililoratibiwa na Mtandao wa Kitaifa wa Wanamichezo wa Kikongo. Mkutano huu wa kwanza kuwahi kufanyika, nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, uliwaleta pamoja waanzilishi wa michezo, wakufunzi wa sanaa ya mapigano, na vijana, wenye ari ya kukua kimwili na kiroho.

Fokasi ilikuwa tafakuri juu ya sheria ya Bwana ya afya, Neno la Hekima, ambalo linawahimiza watoto wa Mungu kuitunza miili yao kama mahekalu ya Roho kwa kuepuka vitu hatarishi na kufuata mtindo wa maisha wenye afya, wenye usawa na wenye nidhamu.

Wakufunzi wakuu walishiriki shuhuda juu ya manufaa ya kuishi kulingana na kanuni hizi. Kupitia maonyesho ya kata, na hadithi binafsi za imani, walionesha kwa mifano jinsi nguvu ya kimwili inavyoweza kudumishwa kwa kufuata njia za Bwana.

Lengo la msingi la mkutano huu lilikuwa kuwapa msukumo vijana, kuwahimiza kufuata mifano iliyowekwa na wanaume na wanawake hawa wa imani, ambao walichanganya pamoja kujikita kwenye riadha na msimamo wa kiroho. Walijifunza kwamba michezo inaweza kuwa chombo cha amani, nidhamu, na huduma na kwa kuheshimu miili yao na kuishi kulingana na mafundisho ya Bwana, wanaweza kufanikisha mambo makubwa na kuwa vyombo katika mikono Yake.

Mtandao wa Kitaifa wa Wanamichezo wa Kikongo ulielezea tamanio la kuona juhudi hii ikivifikia vigingi vyote vya Kinshasha na nje ya Kinshasa. Lengo ni kuzibariki familia nyingi zaidi, kufundisha Neno la Hekima kwa mfano, na kuimarisha imani ya vijana kupitia shughuli ambazo hustawisha mwili na roho.

mkutano huu ulionesha kwa mfano kwamba kwa kuunganisha pamoja nguvu ya kimwili na imani katika Kristo, tunaweza kufikia matokeo mazuri kuliko kawaida. Inapoongozwa na Roho, michezo huwa njia ya utakaso, huduma, na shangwe ya kudumu.