“Uaminifu na Manabii—Waliopita na Waliopo,” Liahona, Jan. 2026.
Uaminifu na Manabii—Waliopita na Waliopo
Kanuni tano muhimu zinaweza kutusaidia kuepuka mtego wa kuwa kinyume na manabii na mitume.
Nilipokuwa na miaka 17, nikiishi Philadelphia Magharibi, Pennsylvania, Marekani, wamisionari waliifundisha familia yangu kuhusu Ono la Kwanza la Joseph Smith. Hamu ya Kijana Joseph ya kuwasiliana na Mungu na kujua mapenzi Yake ilitoa mwangwi wa kina na hamu zangu mwenyewe.
Kama wamisionari walivyotufundisha kuhusu manabii na mitume walio hai, niliuliza, “Je, Kuna Mitume leo? Je, wako wapi?” Walituonyesha picha ya Rais Spencer W. Kimball (1895–1985), washauri wake katika Urais wa Kwanza, na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili mnamo 1980. Hii iliimarisha ushuhuda wangu uliokuwa ukichipua kwamba Mungu, ambaye ni yule yule jana, leo, na milele, bado alihitaji manabii na mitume ili kuwaongoza watoto Wake katika nyakati za sasa.
Baada ya muda, wazazi wangu wote wawili na watoto wote 10 walibatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Tangu nilipowajua manabii na mitume walio hai, ushuhuda wangu juu ya wito na funguo zao takatifu umekua imara zaidi.
Changamoto Zinazowakabili Manabii na Mitume
Kwa kawaida, Shetani daima ametafuta kupunguza kujiamini kwa manabii na mitume. Hata hivyo, kote katika historia wamekuwa mashahidi wakuu wa jina la Yesu Kristo ulimwenguni kote (ona Mafundisho na Maagano 107:23).
Katika wakati wetu, adui anatafuta kuzuia kile Rais Russell M. Nelson alichokiita “kitu muhimu zaidi kinachofanyika duniani leo,” kukusanyika kwa Israeli, ambako lazima kutangulie Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Manabii na mitume wanashikilia funguo za kukusanyika huku. Hivyo, daima wanakabiliwa na upinzani.
Iwe hapo kale au katika siku za mwisho, Shetani hata amepata njia za kudanganya baadhi ya watoto wa Mungu mwenyewe wa agano kupigana dhidi ya Mitume wa Mwanakondoo, waliopita na waliopo sasa (ona 1 Nefi 11:34–36).
Hapa kuna kanuni tano ambazo zinaweza kutusaidia kuepuka kuangukia kwenye mtego huu.
Imani katika Bwana Yesu Kristo
Ya kwanza kati ya kanuni hizi pia ni kanuni ya kwanza ya injili: imani katika Bwana Yesu Kristo na Upatanisho Wake.
Imani ni mwelekeo. Rais Jeffrey R. Holland, Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alifundisha kwamba imani daima inaelekeza kwenye siku zijazo.
Wakati imani yetu katika Kristo na kumtumaini Mungu vinapoongezeka, “tunatazamia kwa jicho la imani, na kuona” ahadi Zao zikitimizwa (ona Alma 5:15; ona pia Mosia 18:21; Alma 32:40). Kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 40 ya “Be One” ya ufunuo wa mwaka 1978 juu ya ukuhani, Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alialika wote “kutazamia katika umoja wa imani yetu na kutumaini katika ahadi za Bwana [ona 2 Nefi 26:33].”
Fokasi hii ya mbele inatupeleka kwenye utimilifu wa ahadi ya Rais Nelson wakati wa tukio kama hili la “amani kamilifu na maelewano” na siku ambapo, kama Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alivyofundisha, “Bwana Yehova atarudi kuishi na wale ambao wamekuwa watu Wake na atawakuta wana umoja, wa moyo mmoja, wameungana pamoja Naye na Baba yetu wa Mbinguni.”
Kinyume chake, Shetani anatafuta kuwashupaza mioyo watoto wa Mungu katika kukwama katika fokasi ya hali ya kuwa nyuma, wakibaki katika hali zilizopita, kauli, au mafundisho—hata yale yaliyofafanuliwa na manabii na mitume wa siku za mwisho. Kama “mshitaki wa ndugu zetu … mchana na usiku” (Ufunuo 12:10), anaanzisha ukosoaji wa kudumu juu ya manabii na mitume wa Mungu na mafundisho yao. Hii kwa ujanja inadhoofisha imani katika kusudi la ushahidi wao, Yesu Kristo—lengo lake kuu ovu sana.
Kauli za umoja, amani, na maelewano kutoka kwa Mitume wa sasa ni wazi kwamba wakati Shetani ni mjanja katika kuchochea ubishi na mfarakano, huu ndio wakati wa watoto wote wa agano wa Mungu (ona 1 Nefi 11:34–36) kuungana katika kukumbatia na kutenda juu ya kweli za milele Mungu anazofunua kupitia manabii na mitume Wake. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuwa na umoja, wenye furaha, wenye nguvu, wa maagano, watu waliojawa na imani na watu wasio na ubaguzi wa rangi, jinsia, kabila au mafarakano mengine.
Mafundisho ya manabii na mitume yanachochea umoja huu na imani ya uhakika katika Yesu Kristo, ambavyo daima vitatusogeza mbele.
Usilaani, Usihukumu, Tenda kwa Imani
Akiona siku zetu, Moroni alifundisha jinsi tunavyoweza kukingwa kutokana na kuwa wakosoaji wa manabii na mitume: kanuni ya kutolaumu au kuhukumu.
“Msinilaani kwa sababu ya mapungufu yangu,” Moroni alisema, “wala baba yangu, kwa sababu ya upungufu wake, wala wale ambao wameandika kabla yake; walakini mshukuruni Mungu kwa sababu amewaonyesha mapungufu yetu, ili mjifunze kuwa na hekima zaidi yetu” (Mormoni 9:31; mkazo umeongezwa).
Kwa maneno mengine, tunafokasi juu ya na kujifunza kutokana na mafundisho ya manabii na mitume na ushahidi juu ya Kristo na injili Yake na kuepuka kutafuta mapungufu yao. Kote katika historia, Mungu amefunua baadhi ya mapungufu haya kwa faida yetu na kutusaidia kujifunza kuwa wenye hekima zaidi. Ninatoa shukurani kwake Yeye kwa kufanya hivyo.
Bado, lazima tuwe waangalifu. Katika mkutano mkuu wa Aprili 2019, Rais Eyring alinukuu fundisho hili la Rais George Q. Cannon (1827–1901), Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza: “Mungu amewachagua watumishi Wake. Yeye anadai kama haki yake kuwalaani, ikiwa wanahitaji laana. Yeye hajatupa idhini sisi mtu mmoja mmoja kuwalaumu na kuwalaani. Hakuna mtu, hata kama ana nguvu namna gani katika imani, hata kama yupo juu vipi katika Ukuhani, anaweza kusema uovu juu ya wapakwa mafuta wa Bwana na kukosoa mamlaka ya Mungu duniani bila kumchukiza Yeye. Roho Mtakatifu atajiondoa kutoka kwa mtu kama huyu, na yeye atakwenda gizani. Jambo likiwa hivi, huoni jinsi ilivyo muhimu kwamba tunapaswa kuwa waangalifu?”
Wewe na mimi tuna baraka na agizo la Bwana kuhusu mafundisho na matendo ya kinabii, ikijumuisha yo yote tunayoweza kuona ni vigumu kuelewa au kuyakubali:
“Nawe utayaangalia maneno yake yote na amri ambazo atazitoa kwenu kadiri atakavyozipokea, mkitembea katika utakatifu wote mbele zangu;
“Kwani neno lake mtalipokea, kama vile linatoka kinywani mwangu mwenyewe, katika uvumilivu wote na imani yote” (Mafundisho na Maagano 21:4–5; msisitizo umeongezwa).
Tena, hatulaani au kuhukumu (ona Mathayo 7:1–2). Kadiri ninavyosonga mbele kwa imani katika Yesu Kristo na shukrani kwa ajili ya baraka za kuwa na manabii na mitume, nimebarikiwa sana (ona Mafundisho na Maagano 21:6).
Epuka Majaribu ya Kuvuka Mamlaka Yetu
Kanuni nyingine muhimu ni kuepuka kuvuka mamlaka yetu au kujichukulia majukumu tusiyokuwa nayo. Mawazo haya yanatudanganya katika kufikiria juu sana ya maoni yetu wenyewe, kitu ambacho kwa kawaida hutokea tunapofikiria kuwa mafundisho ya manabii na mitume ni ya chini sana. Kuwashutumu manabii na mitume, ikijumuisha wale wa zamani, ni wazi tunavuka mamlaka yetu, kwa vile Bwana anabakiza uwezo huu Kwake Yeye Mwenyewe. Nina hakika kabisa kwamba Mwokozi wetu anayejua yote, mwenye upendo, na mwenye rehema ameshughulikia au atashughulikia na kwa hamu kusamehe makosa yoyote au mapungufu ya zamani, kama tunavyotumaini Yeye atatufanyia hivyo kwa wakati huu.
Mfano mwingine wa kuvuka mamlaka yetu ni kudhania kuwaelekeza manabii na mitume kuhusu ni matendo gani Kanisa linapaswa kuchukua au jinsi linavyopaswa kutawaliwa. Hilo ni jukumu la Bwana, sio letu (ona Mafundisho na Maagano 28:2–7). Bila kujali nia njema tunayoweza kuwa nayo, kulaani na kudhania kuwaelekeza manabii na mitume kunatiririka kutoka kwenye kiburi na kusababisha udanganyifu na kushindwa kufuata mamlaka ya kinabii.
Urejesho Unaoendelea
Kuanzia 1820 hadi sasa, Bwana daima amewafunza manabii Wake, waonaji, na wafunuzi katika mchakato wa ufunuo ambao kwa njia hiyo Yeye anaongoza Kanisa Lake.
Rais Nelson alifundisha:
“Tunapokutana kama Baraza la Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, vyumba vyetu vya mikutano vinakuwa vyumba vya ufunuo. Roho ni dhahiri yupo. … Ingawa tunaweza kutofautiana katika mitazamo ya awali, upendo tunaouhisi kwa kila mmoja wetu ni dhabiti. Umoja wetu hutusaidia kutambua mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Kanisa Lake.
“Katika mikutano yetu, walio wengi kamwe sio wanaoamua! Kwa sala tunasikilizana na kuzungumza sisi wenyewe mpaka tunapokuwa tumekubaliana.”
Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Lengo sio tu kuwa na makubaliano miongoni mwa washiriki wa baraza bali ni kupata ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni mchakato unaohusisha vyote sababu na imani kwa ajili ya kupata mawazo na mapenzi ya Bwana.”
Kanuni hii ya usalama iliyorejeshwa, iliyorekebishwa huongeza kujiamini katika uwezo wa viongozi wetu walioko sasa daima kulitawala Kanisa kulingana na mapenzi ya Bwana.
Kuwa na Mtazamo wa Unyenyekevu
Bila shaka, Yesu Kristo anasimama kwenye kichwa cha Kanisa Lake, na Yeye anawaongoza manabii Wake. Kile tunachoweza kuona kama mapungufu katika maneno yao au matendo yao inaweza, kwa kweli, kuonyesha mapungufu katika mtazamo wetu au uelewa wa maisha ya duniani. Kukumbuka kwamba njia za Bwana ni za juu kuliko njia zetu na kwamba mawazo Yake yako juu kuliko mawazo yetu (ona Isaya 55:8–9) inaturuhusu kuepuka kuwahukumu manabii, ikijumuisha wale wa zamani. Mtazamo huu wa unyenyekevu unatuwezesha kutii maneno ya manabii walio hai “katika uvumilivu wote na imani yote” (Mafundisho na Maagano 21:5; ona pia 1:28).
Pia inatusaidia kupokea ongezeko la ufunuo, tumaini, na imani katika Kristo katika ulimwengu unaozidi kuwa mgumu. Yakobo alifundisha, “Kwa hivyo, tunawachunguza manabii, na tunayo mafunuo mengi na roho ya unabii; pamoja na mashahidi hawa wote tunapokea tumaini, na imani yetu haiwezi kutingishwa” (Yakobo 4:6). Kama tu wanyenyekevu, uzoefu huu mtakatifu unaweza kuondoa kutoka kwetu hamu yo yote ya ukosoaji wa manabii na mitume, ikijumuisha wale wa zamani (ona Mafundisho na Maagano 88:124; 136:23). Unyenyekevu hutusaidia “kupekua manabii” kwa ajili ya kweli zinazoongeza shangwe yetu na amani na kutotafuta mapungufu.
Katika roho hiyo, ninatoa ushahidi wangu wa hakika na wa upendo kwamba manabii kutoka Joseph Smith na kuendelea walikuwa manabii wa Mungu katika mfululizo usiovunjika hadi kwa na ikijumuisha Rais Russell M. Nelson. Imekuwa baraka kubwa kwangu “kupekua manabii” na kuja karibu zaidi na Mungu kupitia mafundisho ya kila mmoja wao.
Ninatoa ushahidi kwamba wale walioitwa kwenye utume mtakatifu chini ya maelekezo ya manabii hawa walikuwa na ni mashahidi maalum wa jina la Yesu Kristo ulimwenguni kote. Ni fursa iliyoje kutazama na kusonga mbele hadi kwa Yesu Kristo kupitia mafundisho ya mashahidi hawa.