Liahona
Hajapotea kwa Mwokozi
Januari 2026 Liahona


“Hajapotea kwa Mwokozi,” Liahona, January 2026.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Hajapotea kwa Mwokozi

Nina shukrani kwa baraka ya faraja ambayo ilikuja kutokana na kuhudhuria hekaluni.

kielelezo cha mwanamke akiangalia mchoro wa Yesu Kristo akiwa amembeba mwana kondoo

Kielelezo na Allen Garns, kwa ruhusa ya kuonyesha mchoro wa Del Parson wa Mwanakondoo Aliyepotea

Mwanafamilia na mumewe hivi karibuni waliamua kuacha Kanisa, pamoja na watoto wao wadogo. Habari zilikuwa za kuchosha moyo kwa familia yetu. Kwa kipindi cha wiki chache zilizofuata, tulijaribu kupata kawaida yetu mpya.

Siku zilizofuatia tangazo lao zilijawa na maumivu, machozi, na sala za dhati kwa Baba yetu wa Mbinguni. Mojawapo ya majibu ya haraka kwa maombi yangu lilikuwa kwamba nilihitaji kuabudu hekaluni kila wiki. Kama mwanafunzi na mke na mama anayefanya kazi, nilipata jibu hilo gumu, lakini niliamua kuwa mtiifu kwa msukumo huo kadiri ilivyowezekana.

Jioni moja baada ya mabadiliko magumu ya zamu kazini, nilihisi kwa dhati kwamba nilihitaji kwenda hekaluni usiku ule. Nilimwomba mwanangu aambatane nami ili kufanya kazi ya ibada za mwanzo.

Tulipofika hekaluni, tulikwenda njia zetu tofauti. Nilipokuwa nimefanya kazi kwa niaba ya akina dada kadhaa na kusikiliza baraka zao zilizoahidiwa, nilizidiwa na hisia. Sikuweza kuwaondoa wanafamilia wetu wanao tangatanga akilini mwangu.

Baada ya kumaliza, nilivaa nguo, nikielekea chumba cha kusubiria, na nikaketi chini. Punde, hata hivyo, nilihisi kwamba nilihitaji kubadili viti ili niweze kumwona mwanangu alipotoka kwenye chumba cha kuvalia wanaume.

Nilihama lakini nilihisi kutotulia katika kila sehemu nilipokaa—hadi hatimaye nilipokaa kwenye kochi nikitazama ukuta karibu na mlango wa kuingia hekaluni. Nilikuwa nimetwaa tu maandiko, nikijaribu kutuliza moyo wangu wenye matatizo, wakati nilipotazama juu kuelekea ukutani.

Huko, niliona mchoro wa karibu wa ukubwa wa maisha wa Mwokozi akiwa amembeba mwana kondoo mdogo mikononi Mwake. Roho ghafla alinikumbusha kwamba wakati nilipohisi wanafamilia wangu wapendwa kwangu walikuwa wamepotea, lakini kwa Mwokozi wetu hawakupotea.

“Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotelewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea, hata amwone?

“Naye akiisha kumpata, kwa furaha humbeba mabegani pake, akifurahi.”Luka 15:4–5

Tunaendelea kuwapenda na kuwaombea wale walio tangatanga. Lakini wakati huzuni inaponiosha, nakumbuka uzoefu huu, nikitumaini kwamba siku moja, wale waliopotea watapata njia yao ya kurudi kwa msaada kutoka kwa Mwokozi mwenye upendo.