Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ninawezaje kufokasi zaidi juu ya Mwokozi wakati wa msimu wa Pasaka?
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Maswali na Majibu

“Ninawezaje kufokasi zaidi juu ya Mwokozi wakati wa msimu wa Pasaka?”

mvulana

“Ninafanya juhudi ya kufokasi kwa Mwokozi kwa kusikiliza muziki wenye kuinua, kumfikiria Yeye zaidi, kumtegemea Yeye katika maisha yangu ya kila siku, na kusali sana. Ninapenda kusoma maandiko pia, kujifunza kuhusu Ufufuko Wake na tumaini unaloniletea.”

Maxwell R., 16, Missouri, Marekani

msichana

“Tafuta maandiko ya kusoma pamoja kama familia kila siku au kila wiki ili kukukumbusha juu ya wakati huu muhimu wa maisha ya Mwokozi. Tafuta fursa kila siku za kuwahudumia wengine katika njia kama za Kristo.”

Ahonima A., 15, Tongatapu, Tonga

mvulana

“Ninaweza kufokasi zaidi kwa Kristo kwa kushiriki kitu fulani kumhusu Yeye mtandaoni kila siku.”

Caleb F., 17, Arizona, Marekani

msichana

“Soma maandiko ambayo yanaelezea maisha Yake, hasa wiki ya mwisho kabla ya Kusulubiwa Kwake. Maelezo niyapendayo ni Mathayo 21–27. Kusoma maandiko kunanisaidia kuhisi kuwa karibu zaidi na Mwokozi wangu na kuelewa vyema Upatanisho Wake.”

Grace M.,15, Alberta, Kanada

msichana

“Pasaka na Upatanisho wa Yesu Kristo vinanikumbusha mwanzo mpya na kitu kipya. Kusasisha utaratibu wangu wa kila siku na kutathmini malengo yangu kunanipa nafasi ya kufokasi tena maisha yangu kwa Kristo na kumkumbuka Yeye kwa kukusudia zaidi kwenye kipindi hiki maalum cha mwaka.”

Lilly H., 17, California, Marekani