Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Pasaka Muda Wote
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Pasaka Muda Wote

Fanya Pasaka kuwa kipindi cha tumaini kwa kusogea karibu na Mwokozi.

picha za vijana wakifanya shughuli mbalimbali, ndani ya saa

Vielelezo na Toby Newsome

Katika Jumapili ya kwanza ya Pasaka, wakati Mariamu Magdalena na wanawake wengine walipotembelea kaburi la Kristo, malaika waliwaambia, “Hayupo hapa, kwani amefufuka” (Mathayo 28:6). Ujumbe huu ulileta matumaini mengi kwa wanafunzi Wake baada ya kukata tamaa kwa kushuhudia Kusulubiwa Kwake.

Habari bora zaidi? Ujumbe huo bado ni wa kweli. Kristo bado amefufuka. Bado ni mshindi juu ya kifo na dhambi. Na tumaini ambalo linakuja kutokana na Ufufuko Wake bado linapatikana kwako—sio tu kwenye Pasaka, bali wakati wote!

Pasaka sio siku pekee unayoweza kuheshimu Ufufuko. Jaribu baadhi ya mapendekezo haya kuifanya Pasaka—na sherehe zake kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake na Ufufuko—kuwa kipindi cha tumaini na furaha.

Jifunze Maisha ya Mwokozi

Maandiko ni nyenzo yenye nguvu sana ili kukusaidia kumjua Yesu Kristo binafsi na kuimarisha imani yako Kwake. Wakati wa msimu wa Pasaka, unaweza kufokasi kujifunza kwako maandiko katika wiki ya mwisho ya maisha Yake au katika matembezi Yake kule Mabara ya Amerika kama Mwokozi wa ulimwengu aliyefufuka. Kusoma matukio haya yenye nguvu kunaweza kukusaidia kuhisi upendo wa Mwokozi kwako na kuelewa vyema Upatanisho Wake na Ufufuko Wake.

Kama hauna uhakika ni vifungu gani vya kufokasia, ungeweza kujaribu kufuata mwongozo wa kujifunza wa Pasaka katika Njoo, Unifuate au miongozo mingine ya kujifunza iliyochapishwa kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Shiriki katika Kazi ya Hekaluni

Ushindi wa Kristo dhidi ya kifo na ufahamu kwamba sisi pia tutafufuliwa ni “jumbe tukufu zaidi kuliko zote kwa wanadamu.” Kwa sababu ya Upatanisho na Ufufuko Wake, familia zetu zinaweza kuwa za milele, na mababu zetu wote wanaweza kupata fursa ya kufanya maagano matakatifu.

Unaweza kusherehekea Ufufuko wa Yesu Kristo na kuendelea na kazi Yake ya kuwakomboa wale walio katika gereza la kiroho (ona 1 Petro 3:18–20) kwa kufanya historia ya familia na kazi ya hekaluni. Huduma yako hekaluni inaruhusu roho hizo kuchagua kupokea baraka zote za Upatanisho wa Kristo pia.

Wahudumie Wengine kama ambavyo Kristo Angewahudumia

Yesu Kristo aliwainua na kuwahudumia wengine katika huduma Yake yote ya duniani—hata akiwa msalabani. Unaweza kuheshimu mfano Wake kwa kuwahudumia watu walio kuzunguka jinsi ambavyo Yeye angefanya. Hata matendo rahisi ya ukarimu kama vile kutabasamu mara kwa mara, kuwasikiliza wengine kwa dhati, na kusaidia nyumbani kunaweza kutengeneza mazingira ya upendo kama wa Kristo. Unapowahudumia wengine, wote wewe na wao mnaweza kuhisi tumaini na uzuri wa msimu wa Pasaka.

Pokea Sakramenti Kwa Kukusudia

Mwokozi Mwenyewe alianzisha desturi ya kukusaidia kumkumbuka Yeye vizuri zaidi kuliko kitu kingine chochote: sakramenti. Kushiriki sakramenti kunaonyesha kwamba uko tayari “daima kumkumbuka na kushika amri zake,” na kama malipo Yeye anaahidi kwamba “daima Roho wake atakuwa pamoja [nawe]” (Mafundisho na Maagano 20:77). Hiyo ni ahadi yenye nguvu! Unashiriki sakramenti kila wiki, unaweza kuanza kuhisi ukweli wa ahadi hiyo wakati wa Pasaka na daima.

Jaribu kutafakari juu ya huduma ya Yesu Kristo, Upatanisho, na Ufufuko unaposhiriki sakramenti. Omba kwa dhati, na ujaribu kufikiria kuhusu jinsi dhabihu Yake ilivyokubariki wewe binafsi.

Muhtasari

  1. Dallin H. Oaks, Facebook, Jan. 2, 2025, facebook.com/dallin.h.oaks.