Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Kumsherehekea Mwokozi
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Sauti za Vijana

Kumsherehekea Mwokozi

familia kwenye Pasaka

Kielelezo na Katelyn Budge

Napenda Pasaka. Ninapenda kujumuika pamoja kama familia kumsherehekea Yesu Kristo akifufuka kutoka kwa wafu. Kutumia muda na familia yangu daima ni kitu ambacho kwa kweli ninakifurahia, lakini kufikiria kuhusu mambo yote ambayo Mwokozi ametutendea ni ya kupendeza zaidi.

Tunapojiandaa kwa ajili ya kuwinda yai letu la Pasaka, tunaweka maandiko ndani ya mayai. Tunasoma maandiko tunapoyapata wakati wa kuwinda. Wakati fulani, tulitengeneza kaburi dogo. Kisha tukaandika hofu zetu zote, tukaziweka ndani ya kaburi, na kuweka jiwe mbele yake. Siku iliyofuata, karatasi zote zilikuwa zimeondolewa—zikitukumbusha jinsi Mwokozi anavyoweza kutusaidia na hofu zetu.

Yesu Kristo ni Rafiki yangu mkamilifu, wa Mbinguni. Ninajua kwamba bila kujali chochote, Yeye daima atanielewa.

msichana

Zoi S., 17, Bavaria, Ujerumani

Hufurahia kucheza densi, tenisi, na kujishughulisha.