Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Sherehe za Pasaka: Ukweli Mtupu
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Sherehe za Pasaka: Ukweli Mtupu

Hapa ni baadhi ya mambo ambayo huenda hujayajua kuhusu sherehe za Pasaka.

Kuingia kwa ushindi Kwa Yesu Kristo ndani ya Yerusalemu

Kuingia kwa Ushindi Kwa Kristo ndani ya Yerusalemu, na Harry Anderson

Unajua nini kuhusu Pasaka? Pengine unajua sehemu muhimu zaidi: Ni sherehe ya dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo na Ufufuko.

Kunaweza kuwa na baadhi ya maswali uliyonayo kuhusu Pasaka na jinsi inavyo sherehekewa na watu wengi, vile vile kwa nini tunafokasi juu yake jinsi hiyo. Haya ni majibu ya maswali machache kama hayo.

Jumapili ya Matawi na Wiki Takatifu ni nini?

Wiki Takatifu husherehekea wiki ya mwisho ya huduma ya Yesu Kristo duniani. Jumapili ya Matawi ni siku ya kwanza ya Wiki Takatifu. Inasherehekea siku ya kuingia kwa Shangwe kwa Yesu Kristo Yerusalemu, akiwa amepanda punda mdogo, katika kutimiza unabii. Watu walisambaza matawi ya mitende na nguo ardhini mbele Yake, wakipiga kelele, “Hosana.” (Ona Mathayo 21:6-11.) Hii ilitokea wiki moja kamili kabla ya Ufufuko wa Yesu Kristo, ambayo inasherehekewa siku ya Pasaka, siku ya mwisho ya Wiki Takatifu. Wiki hii pia inajumuisha Ijumaa Kuu (kuadhimisha kusulubiwa na mazishi ya Kristo).

Yesu Kristo akiwa Gethsemane

Kristo katika Gethsemane, na Dan Burr

Ni lini Wakristo walianza kusherehekea Pasaka?

Rekodi ya mwanzo kabisa ya kuwa na sherehe ya Pasaka ya aina yoyote inatoka katikati ya karne ya pili (wakati mwingine kati ya 160 na 170 B.K.). Hata hivyo, Wakristo labda walikuwa wakiadhimisha Kusulubiwa na Ufufuko wa Yesu Kristo kwa namna fulani tangu nyakati za awali kabisa. Kwa sababu wale wanaomfuata Yesu Kristo wanaamini kazi Yake ya upatanisho, ambayo kilele chake huitimishwa na Ufufuko, ni tukio muhimu zaidi katika historia ya wanadamu wote, inaleta maana kwamba wangesherehekea matukio haya tangu siku za mwanzo kabisa wa Ukristo. Leo tunaweza kusherehekea Upatanisho na Ufufuko wa Kristo kila Jumapili tunapopokea sakramenti.

Kwa nini tarehe ya Pasaka ni tofauti kila mwaka?

Ni ngumu kidogo, lakini hesabu ya msingi kwa Jumapili ya Pasaka ni: Ni Jumapili ya kwanza baada ya “mwezi kamili wa pasaka,” ambayo ni mwezi kamili wa kwanza baada ya ikwinoksi ya majira ya kuchipua katika Ulimwengu wa Kaskazini wa ikweta (Machi 21). (Kwa kweli ina tatanisha zaidi kuliko hivyo, lakini hii itafaa.)

Sababu ya fomula hii inahusiana na kweli mbili: (1) Kusulubiwa kwa Mwokozi kulitokea wakati wa Pasaka, na (2) Ufufuko Wake ulitokea siku ya kwanza ya wiki (Jumapili).

Wakristo wa mwanzo walijadili kama ilikuwa muhimu zaidi kusherehekea Pasaka katika Pasaka au Jumapili. Pasaka ni sherehe ya Kiyahudi iliyofungwa kwenye kalenda ya Kiebrania, ambayo ni kalenda ya jua ambayo haiendani na kalenda ya mwezi ambayo watu wengi hutumia. Kwenye kalenda ya Kiebrania, Pasaka inasherehekewa siku ya 14, ya mwezi wa saba. Pamoja na, kila baada ya miaka miwili au mitatu, inaongeza mwezi wa ziada kukaa katika kusawazisha na misimu. Kwa hiyo, kuiunganisha Pasaka na Pasaka ya Kiyahudi ilimaanisha kwamba tarehe ingeruka karibu sana na mara chache tu kuwa Jumapili.

Ili kutatua swali, baraza la Kikristo miaka 325 Baada ya Kristo liliamua kuunganisha tarehe ambayo Pasaka ina sherehekewa.

Hivyo, hadithi ndefu kuwa fupi: Kulingana na hesabu iliyotumiwa na Wakristo wengi, Jumapili ya Pasaka inaweza kuja mapema kama Machi 22 au kuchelewa kama Aprili 25.

Chakula cha Mwisho

Kwa Ukumbusho Wangu, na Walter Rane

Ni kwa jinsi gani sungura na mayai vilikuja kuhusishwa na Pasaka?

Sungura wa Pasaka (au wanyama wengine) wakitoa mayai yalianza kujitokeza Ulaya katika karne ya 17. Mambo haya hayakuwa ya kawaida mpaka karne ya 19. Inaaminika kwamba watu waliwaazima kutoka kwenye ishara zisizo za Kikristo za wakati wa majira ya kuchipua, kufanywa upya, na maisha na kisha kuwaunganisha kwenye Pasaka na Ufufuko wa Yesu Kristo.

Yesu Kristo akitoka kaburini

Yesu Akitoka Kaburini, na Dan Burr

Kwa nini tunafokasi sana kwenye Pasaka?

Urais wa Kwanza umetuomba tuinue Sherehe zetu za Pasaka. Bila kujali kile wengine wanachoamini au kufanya, tunapaswa kusherehekea Ufufuko wa Mwokozi wetu aliye hai kwa kujifunza mafundisho Yake na kusaidia kukuza tamaduni za Pasaka katika jumuiya zetu kwa ujumla, hususani ndani ya familia zetu. Tunawapa changamoto ya kufanya hivyo” (Dallin H. Oaks, “Amefufuka!: Ujumbe Maalum wa Msimu wa Pasaka kutoka kwa Urais wa Kwanza” [video], Gospel Library).