Ninawezaje Kuwasaidia Marafiki na Familia Yangu?
Kama mtu aliyefufuka, Yesu Kristo aliwatembelea Wanefi na kuwaalika kufanya kitu ambacho kiliweka mpangilio kwa ajili ya kile ambacho sisi kama wanafunzi Wake wa sasa pia tunaweza kufanya. Alisema:
“Mnao wowote ambao ni wagonjwa miongoni mwenu? … Mnao wowote ambao ni viwete, au vipofu, … au ambao wanateseka kwa njia yoyote? Waleteni hapa na nitawaponya, kwani ninayo huruma juu yenu” (3 Nefi 17:7).
Zingatia namna wale wanafunzi wa kale walivyoitikia.
“Umati wote … ulisonga mbele na wagonjwa wao … na wote waliosumbuka kwa jinsi yoyote; na akawaponya” (3 Nefi 17:9).
Ninajua kwamba Yesu Kristo yu hai na kwamba Yeye bado ni Mponyaji mnyenyekevu. Tunapoitikia mwaliko Wake wa kuwaleta marafiki na familia zetu Kwake, Yeye atawaponya kwa njia Yake mwenyewe.
“Na wote, ambao walikuwa wameponywa, na wale ambao walikuwa wazima, waliinama chini miguuni mwake, na kumwabudu.” (3 Nefi 17:10)
Kila mmoja na aje kwa Kristo tunapowaleta wengine Kwake msimu huu wa Pasaka.
Kwa upendo,
Sean R. Dixon
Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Wavulana