Hosana Yangu
Kila mmoja wetu ana kitu maishani mwetu ambacho hutufanya kupiga magoti.
Mojawapo ya sura ninazozipenda za Agano Jipya inazungumza kuhusu kuingia kwa shangwe ya ushindi kwa Yesu Kristo katika Yerusalemu. Watu walipaza sauti, “Hosana, kwa Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni” (Mathayo 21:9). Wakati wowote ninaposoma hili, nafikiri: Hosana yangu ni nini?
Nimekuwa na kusitasita maishani yangu mwote. Wakati mwingine nimehisi kufadhaika sana na kukata tamaa kwa sababu sikuweza kujieleza jinsi nilivyotaka kufanya hivyo. Ningependa ama kuzungumza kikamilifu au kamwe kutozungumza tena. Siku zote nina wasiwasi ninapoongea mbele ya wengine au hata ninaposali kwa sauti kubwa. Kimya kimya nimesihi kwa ajili ya subira, amani, na msaada mara nyingi. Hii ni mojawapo ya hosana zangu binafsi—kilio changu cha ukombozi.
Kama vile Kristo hakupuuza vilio vya watu katika Yerusalemu, Hajawahi kupuuza cha kwangu. Hajaondoa kusitasita kwangu, lakini Ameniimarisha kwa njia ambazo sikutarajia. Amenisaidia kuhisi amani katika nyakati za wasiwasi na kutambua kwamba sauti yangu, yenye dosari kama inavyoweza kuwa, inatosha Kwake.
Kila mmoja wetu ana kitu maishani mwetu ambacho hutufanya kupiga magoti. Wakati mwingine, tunaweza kuhisi kwamba vilio vyetu havijibiwi. Lakini Yeye husikia kila hosana. Na katika njia Yake kamilifu na wakati Wake mkamilifu, Yeye atakuja kutusaidia.
Katika Gethsemane, Kristo aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu na kuhisi maumivu yetu na mapambano yetu. Anaendelea kuwaongoza na kuwafariji wote wanaomgeukia Yeye na Baba wa Mbinguni. Kristo yule yule ambaye aliteseka kwa ajili yetu katika Gethsemane na msalabani pia alifufuka kutoka kaburini, akishinda kifo ili kwamba tuweze kuwa na tumaini. Ufufuko Wake ni jibu la mwisho kwa kila hosana.
Mwandishi anaishi California, Marekani.