Sauti za Vijana
Ninaweza Kumwalika Kila Mtu
Kielelezo na Katelyn Budge
Inanifanya niwe na wasiwasi kushiriki injili na marafiki lakini pia mwenye furaha na mwenye kusisimka. Kila mwaka, tunawinda yai la Pasaka nyumbani kwetu. Tunawaalika wamisionari na marafiki zetu ambao si waumini wa Kanisa.
Pia mara nyingi ninawaalika marafiki zangu kuja kanisani au kwenye shughuli za vijana. Rafiki mmoja tu amekuja kwenye shughuli, na hakuna aliyekuja kanisani—bado. Lakini ninaendelea kuwaalika ili waweze kumkaribia Mungu na kuishi Naye tena. Inanifanya niwe na furaha kuwahudumia wengine kwa kuwaalika kuja kwa Kristo.
Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wetu, Mwanakondoo wa Mungu, na Mchungaji Mwema. Ninajua kwamba tutaweza kuishi na Mungu tena kama tutamfuata Yeye.
Akon C., miaka 13, Hawaii, Marekani
Anapenda kucheza michezo, kukimbia mbio, na kujenga vitu.