Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Pasaka‑Inayojikita kwa Mwokozi
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


PasakaInayojikita kwa Mwokozi

Na Maisha Yanayojikita kwenye Pasaka

Sote tunaweza kufikia nguvu ya Mwokozi ya faraja na mabadiliko.

mvulana

Picha na Janae Bingham

Katika seminari, tulizungumza kuhusu maana halisi ya Pasaka na jinsi tunavyopaswa kuisherehekea. Siyo tu kuhusu pipi na sungura—ni kuhusu Mwokozi. Nilijiuliza mwenyewe, “Ni desturi gani za Pasaka ninazoweza kuanza nyumbani kwangu ambazo zinafokasi zaidi juu ya Mwokozi?”

Yesu Kristo

Ninapenda kujenga vitu na matofali ya LEGO® Nilipata picha ya Mwokozi kutoka kwenye Maktaba ya Injili mtandaoni na iligeuzwa kuwa maelekezo ya tofali. Nilifanyia kazi picha ya tofali wakati nikisikiliza mkutano mkuu. Nilipomaliza, niliitundika nyumbani kwangu.

familia mezani

Kutoa Michoro ya Mwokozi

Pia nilinunua sanduku kubwa la sanamu ndogo za Yesu Kristo kwa ajili ya Pasaka. Mwanzoni nilikuwa nikienda kuzificha zote shuleni kwangu. Lakini wakati watu shuleni walipoliona sanduku, waliziomba hizo sanamu ndogo. Walimu walianza kuuliza pia. Na kisha watoto ambao sikuwahi kufikiria wangetaka sanamu ndogo za Yesu waliomba. Na hivyo nilizitoa kwa kila mtu niliyemwona.

mvulana akicheza gitaa la wima la besi mbili

Mwokozi hakuogopa kuzungumza na mtu yeyote, hata watu waliotengwa na jamii Yake. Alikuwa rafiki pamoja nao. Alitumia muda pamoja nao. Alikula pamoja nao. Kugawa visanamu vidogo kulinifundisha kuwa mwenye kujitoa zaidi, kama vile Mwokozi alivyokuwa. Pia ilinifundisha kwamba bila kujali wewe ni nani, bila kujali unafikiri umefanya nini, daima kuna nafasi kwa ajili ya Yesu Kristo katika maisha yako.

Kubadilika Kupitia Mwokozi

Maisha yangu yote nimejiuliza, ninawezaje kupata Upatanisho wa Mwokozi? Lakini Pasaka hii, nilijifunza kwamba ikiwa nitafanya mabadiliko katika maisha yangu kuwa zaidi kama Mwokozi, neema Yake ya upatanisho inafanya kazi katika maisha yangu. Na kama nikijaribu kila siku kubadili vitu vidogo, basi nitaanza kuwa bora.

Kwa miaka michache katika maisha yangu, nilipambana na matumizi ya ponografia. Baada ya somo katika seminari, nilivutiwa kuzungumza na askofu wangu. Ilikuwa rahisi sana kuanza kushinda pambano langu mara hatimaye nilipomwambia askofu wangu na wazazi wangu, kwa sababu ni vigumu sana kupitia hilo peke yangu.

mvulana akisali

Nilianza kujaribu kusali na kusoma maandiko yangu kila siku, na nilijaribu kuwa mkarimu shuleni. Ilinisaidia kwa sababu nilikuwa nikifokasi zaidi kwa Mwokozi kuliko dhambi zangu. Nilimgeukia zaidi Yeye kuliko pale nilipokuwa hapo zamani.

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, nimeshinda pambano langu na ponografia. Nimekuwa zaidi yule ambaye Mungu anahitaji niwe. Sasa ninaweza kubariki sakramenti kwa sababu Mwokozi ananibadilisha na kunisafisha. Ninashukuru kuwa mwenye kustahili kutumia ukuhani ili kubariki maisha ya wale wanaonizunguka.

familia ikijifunza maandiko

Kuunganisha Pasaka na mimi

Mwaka huu wakati wa seminari, nilikuwa na uzoefu mzuri sana wakati tulipokuwa tunazungumza kuhusu dhabihu ya Mwokozi. Nilikuwa na wazo kwamba wakati alipokuwa akiteseka, Angeweza kusimamisha mateso wakati wowote. Lakini kisha nikamfikiria yeye akifikiria, “hapana, nahitaji kuendelea kufanya hili. Ninahitaji kufanya hili kwa ajili ya Ben. Yeye anahitaji hili.” Kwangu mimi, wazo hilo liliunganisha tu uhusiano wangu na Mwokozi kwenye Pasaka.

familia

Pasaka ijayo, pengine nitafanyia kazi picha nyingine ya matofali ya Yesu. Mimi kwa hakika nataka kugawa visanamu vidogo. Kwa njia yoyote ile, nitakuwa nikifikiria kuhusu mateso ya Kristo na Upatanisho Wake kwa ajili yangu. Kwa sababu Yake, ninaweza kutubu dhambi zangu na kurudi Kwake na kwa Baba wa Mbinguni siku moja.

Ninajua kwamba Mwokozi aliishi na kufa kwa ajili ya kila mmoja wetu binafsi na kwamba Yeye anajua sisi ni akina nani na kile tunachohitaji. Kama kweli tunajaribu, tunaweza kufikia nguvu Zake za faraja na mabadiliko, na tunaweza kuwa watu bora.

Mwandishi anaishi Idaho, Marekani.