Sehemu yaBurudani
Vielelezo na Mark Robison
Tamaduni za Pasaka Fumbo la Kimantiki
Vijana sita wana kwenda sokoni muda mfupi kabla ya Pasaka. Ukitumia picha na vidokezo, linganisha kila kijana kwa desturi ya Familia yao ya Kikristo yenye kiini cha desturi ya Pasaka. (Ona ukurasa wa 16 ili kupata jinsi tamaduni hizi zinavyoweza kujikita kwa Mwokozi!)
-
Ella
-
Daudi
-
Frieda
-
Juan
-
Giulia
-
Oliver
Tamaduni:
-
Kurusha tiara
-
Kusuka majani ya mtende
-
Kuwasha moto mkubwa
-
Kupaka rangi mayai
-
Kutengeneza na kuvunja mayai yaliyojazwa chengechenge za rangi mbalimbali
-
Kula mkate maalum
Vidokezo:
Kijana anayepanga kuwasha moto mkubwa ni rafiki wa kijana anayerusha tiara.
Kijana anaye tengeneza mkate maalum ana mbwa.
Kijana anayesuka majani ya mitende hupenda ndizi.
Ella anahitaji mayai mengi kwa ajili ya sherehe yake.
Kwa kusherehekea kwake, Daudi anatarajia upepo fulani.
Mvulana anatengeneza mayai yaliyo jazwa chengechenge zenye rangi mbalimbali.
Tiara za kustaajabisha
Huko Bermuda, watu wengi wanarusha tiara wakati wa Pasaka kumkumbuka Kristo akiinuka kutoka kaburini. Tiara ipi inarushwa na kijana?
1.
2.
3.
Shindano la Haiku
haiku ni aina ya mashairi ya Kijapani yenye mistari mitatu tu. Mstari wa kwanza ni silabi tano, mstari wa pili ni silabi saba, na mstari wa tatu ni silabi tano. (Kama hujui “silabi” ni nini, muulize mama yako, au mtu mwingine mwerevu.)
Sasa ni zamu yako! Andika haiku ya Pasaka kuhusu dhabihu ya Mwokozi au Ufufuko. Upatanisho Wake una maanisha nini kwako?
Tuma barua pepe yako ya haiku (katika lugha yako ya asili) kwa fstoy@ChurchofJesusChrist.org kwa ajili ya nafasi ya kujumuishwa!
Vichekesho
Unaona, David, ninaweza kukupa samaki na kukulisha kwa siku moja, au ninaweza kukufundisha kuvua samaki na kukulisha maisha yote!
Je, Baba hatuwezi kwenda tu kupata pizza, ?
Ryan Stoker
Majibu
Tamaduni za Pasaka Fumbo la Mantiki: 1D, 2A, 3C, 4E, 5B, 6F
Tiara za kustaajabisha: Tiara iliyo rushwa na kijana ni tiara 1.