Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Pasaka Yetu—Sakramenti
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Njoo, Unifuate

Kutoka 12

Pasaka Yetu—Sakramenti

Kuna mfanano kati ya Pasaka ya kale na sakramenti yetu ya kila wiki.

msichana

Vielelezo na Alyssa Tallent

Kabla ya Waisraeli wa kale kuondoka toka utumwani huko Misri, waliombwa kutii maelekezo mahususi kutoka kwa Bwana ili kwamba malaika mwangamizaji aweze kuwaacha, au kuwapita (ona Kutoka 12). Baada ya kuondoka Misri, Waisraeli wali adhimisha karamu kila mwaka, iliyoitwa Pasaka, kukumbuka jinsi Bwana alivyowakomboa watu Wake wa agano.

Wakati wa wiki ya mwisho ya maisha Yake duniani, Yesu Kristo alikuwa kwenye chakula cha Pasaka. Sasa tunaita chakula hicho karamu ya mwisho. Mwokozi alitumia tukio hilo kutambulisha ibada ya sakramenti, ambayo sasa tunaishiriki kila wiki. (Ona Mathayo 26:26-28; Luka 22:-19–20; Mafundisho na Maagano 20:77—79).

Hapa kuna mifanano miwili kati ya Pasaka ya kwanza, Karamu ya Mwisho ya Bwana, na sakramenti ya leo ambayo inaweza kutusaidia kukumbuka ukombozi wetu kupitia Mwokozi.

kingo za mlango wakati wa Pasaka
Karamu ya Mwisho
mkate na maji ya sakramenti

Mkate

Pasaka: Kwa siku saba, Waisraeli walikula mkate usiotiwa chachu (ambao ni rahisi kuutengeneza na ambao huchelewa kupata uharibifu na kuoza.)

Karamu ya Mwisho: Yesu Kristo alibariki na kumega mkate usiotiwa chachu wa Pasaka, na akawapa wanafunzi. Aliwaambia wale kwa ukumbusho wa mwili Wake, ambao Alijua punde ungevunjika na angekufa lakini angefufuka tena.

Sakramenti: Tunakula mkate kwa ukumbusho wa mwili wa Yesu Kristo.

Yesu Kristo ni Mkate wa uzima. Kupitia Ufufuko Wake, sisi sote tutafufuliwa na miili mikamilifu, isiyooza, miili isiyo haribika. Yeye hutukomboa kutokana na kifo.

Damu ya Mwanakondoo

Pasaka: Mwanakondoo wa Pasaka alikuwa mwanakondoo asiye na dosari, dume mwenye umri wa mwaka mmoja. Alichinjwa, na damu yake ilikusanywa katika bakuli. Hyssop (mmea) ulichanganywa kwenye bakuli na kutumika kueneza damu kuzunguka kingo za mlango wa nje wa nyumba. Hii ilikuwa ishara ya nje ya kutambua watu wa agano wa Bwana kupitwa na malaika mwangamizaji ili waweze kukombolewa kutoka utumwani Misri.

Karamu ya Mwisho: Yesu Kristo alitumia divai kuwakilisha damu Yake. Aliwaambia wanafunzi Wake wainywe kwa ukumbusho wa damu Yake, ambayo ingemwagwa kwa ajili yao kwa ondoleo la dhambi na kama sehemu ya agano jipya.

Sakramenti: Tunakunywa maji kwa ukumbusho wa damu ya Yesu Kristo.

Yesu Kristo ni Mwanakondoo wa Mungu. Damu yake ilimwagwa alipoteseka kwa ajili ya dhambi na udhaifu wetu. Damu Yake—dhabihu Yake—inatutakasa. Yeye hutuokoa kutokana na dhambi.