Unganika
Fabio P.
16, Salzburg, Austria
Picha na Ashlee Larsen
Katika Pasaka, kwa kawaida tunakutana pamoja na familia yetu yote, takribani watu 30 hadi 40. Nilipokuwa mdogo, nilitazamia kikapu chenye mayai na chokoleti. Na ile ilikuwa ya kufurahisha sana. Lakini siku hizi, nina fokasi zaidi juu ya maana ya Pasaka.
Kanisani, tunazungumza kuhusu Pasaka sana. Na katika kujifunza kwangu maandiko, ninafokasi zaidi juu ya kile kilichotokea wakati wa Pasaka. Ninafikiria kuhusu Yesu Kristo na kile alichofanya kwa ajili yetu, na ninajisikia muunganiko imara na Yeye.
Andiko langu nilipendalo ni 3 Nefi 15:9. Lina sema, “Tazama, Mimi ndiye sheria, na nuru. Nitazameni mimi, na mvumilie hadi mwisho, na mtaishi; kwani kwa yule ambaye huvumilia hadi mwisho nitampa uzima wa milele.”
Kama nitaendelea kujitahidi kuchagua mema katika maisha yangu, kama ninavyofanya sasa hivi, ninaweza kurudi Kwake na kuwa na uzima wa milele.