Hadithi kutoka Agano la Kale
Mwanzo 37–47
Aliuzwa Misri
Yusufu
Vielelezo na Katy Dockrill
Hadithi Yake
Koti
Yusufu alikuwa mtoto mpendwa wa Yakobo. Yakobo alimtengenezea Yusufu koti maalum. Kaka zake Yusufu walimwonea wivu. (Haikuwapendeza kwamba Yusufu alioteshwa ndoto zilizokuwa na mwongozo wa kiungu kutoka kwa Mungu kwamba siku moja angewatawala.)
Usaliti
Kaka zake Yusufu walimuuza kwa watu waliokuwa wakienda Misri na kumwambia Yakobo kwamba Yusufu alikuwa amefariki. Huko Misri, Yusufu alikuwa mtumwa na alitupwa gerezani kwa kosa ambalo hakufanya. Daima alikuwa mwaminifu kwa Mungu, na Bwana alikuwa pamoja naye na akambariki.
Baa la Njaa
Hatimaye, Yusufu alitafsiri ndoto ya Farao na kumpa ushauri wa kujiandaa kwa ajili ya njaa ijayo. Farao alimfanya Yusufu kuwa mtawala huko Misri. Punde, kaka zake walikuja Misri kununua nafaka. Hawakutambua kuwa walikuwa wakiomba msaada kutoka kwa ndugu waliyekuwa wamemuuza!
Ukombozi
Yusufu hatimaye alijifunua mwenyewe kwa kaka zake na kuwapa chakula na makazi huko Misri. Aliwasamehe na kuokoa familia yake. Kaka hawa hawa wakawa makabila 12 ya Israeli.
Hadithi Yako
Kama Yusufu, unaweza kuwa na siku ambazo unahisi kusalitiwa au kuumizwa. Matendo ya watu wengine yanaweza kuwa na matokeo makubwa. Lakini unapokuwa mwaminifu kwa Mungu na kujaribu kuwasamehe wengine, utaimarishwa na kubarikiwa.