Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Kusherehekea Pasaka
Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana Machi 2026


Kusherehekea Pasaka

Wakati Tunapokumbuka haya Yote Ni Juu Ya Nani

Desturi 6 za Pasaka kutoka ulimwenguni kote na jinsi zinavyoweza kutusaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Mayai ya Pasaka

Vielelezo na Judy Bloomfield

Desturi

Uhusiano kwa Kristo

1. Mayai ya Pasaka

Mayai, mayai, mayai. Kote ulimwenguni, mayai ya Pasaka yanapambwa, yanatafutwa, yanaviringishwa, yana pasuliwa, na kuliwa. Katika Ujerumani na Austria, mayai ya Pasaka huwekwa kwenye miti (Ostereierbaum). Huko Mexico, mayai yana tobolewa na kujazwa na confetti (cascarone) na kisha kuvunjwa juu ya kichwa cha mtu.

Kwa hakika, watu wengi hutumia mayai kusherehekea Pasaka bila kufokasi kwa Mwokozi kabisa. Ni juu yetu kufokasi kwa Mwokozi katika desturi zetu za Pasaka. Mayai yanaweza kuwa ishara za maisha mapya, muungano haraka kwenye ufufuo. Rangi nyekundu imekuwa ikitumika katika baadhi ya tamaduni kuwakilisha dhabihu ya Mwokozi. Na wakati yai linapopasuka, ganda linaweza kutukumbusha juu ya kaburi tupu na Mwokozi Aliyefufuka. Kama ikiwa hujawahi kuunganisha tamaduni zako za Pasaka Kwake, sasa ndio wakati wa kuanza!

2. Mioto yta Pasaka

Kuwa na moto mkubwa wa sherehe ni desturi ya kawaida ya Pasaka hususan katika Ujerumani, Uholanzi, Croatia, na Ufini.

moto

Moto wakati wa Pasaka unaweza kutukumbusha kumtazama Mwokozi, ambaye huleta nuru na joto ulimwenguni na ni, kwa kweli, Nuru ya Ulimwengu Mwenyewe (ona Yohana 8:12).

3. Vyakula Maalum

Kote ulimwenguni wakati wa pasaka, vyakula viwili vyenye ishara huliwa tena na tena: mwanakondoo na mkate.

mkate na kipande cha nyama ya kondoo

Mwanakondoo anaweza kumwakilisha Mwanakondoo wa Mungu—Mwokozi Mwenyewe. Mkate unaweza kutukumbusha juu ya Yesu Kristo, ambaye ni Mkate wa Uzima (ona Yohana 6:35).

4. Kupunga tawi la Mitende

Katika baadhi ya nchi, kama vile Italia, Uhispania, Ufilipino, Mexico, Misri, na Ethiopia, watu hutengeneza majani ya mitende au mimea mingine katika Jumapili ya Matawi.

Kuti la mitende

Jumapili ya Matawi ni Jumapili kabla ya Pasaka na inasherehekea kuingia kwa Yesu kwa shangwe Yerusalemu, wakati watu wanaposambaza matawi ya mitende mbele Yake.

5. Kurusha Tiara

Huko Bermuda wakati wa Pasaka, watu hurusha tiara za rangi!

tiara

Desturi hii ni ukumbusho wa burudani ya Ufufuko wa Mwokozi na jinsi Yeye baadaye alivyoinuka juu mbinguni.

6. Ibada ya Kanisa

Usisahau mojawapo ya desturi muhimu za Pasaka—kwenda kanisani! Tunaenda Kanisani Jumapili ya Pasaka kushiriki sakramenti na kumkumbuka Mwokozi. (Kama mkutano mkuu upo siku ya Pasaka, tunaweza kumkumbuka Yeye kwa kusikiliza—kisha kushiriki sakramenti tena wiki inayofuata.)

mkate wa sakramenti na maji

Tunaposhika maagano yetu na kuyafanya upya kupitia sakramenti, tunabarikiwa daima kuwa na Roho pamoja nasi. Hii inaweza kutusaidia kuunganika na Mwokozi kwenye Pasaka na siku zingine, vile vile.

Vijana Wanaojihusisha: Tamaduni Binafsi za Pasaka

“Ninatoa mayai ya Pasaka ya chokoleti kwa wamisionari katika kata yangu.”

Jennyfer M., umri miaka 23, Pernambuco, Brazil

“Familia yetu ilifanya chakula cha jioni cha mwisho, na tulijaribu kukifanya kitamaduni iwezekanavyo.”

Alice F., umri miaka 16, Utah, Marekani

“Mimi na familia yangu tunakwenda makaburini, kuimba nyimbo za dini pamoja, na kutoa shuhuda zetu.”

Rachel G., umri miaka 19, Virginia, Marekani

“Nilienda hekaluni wakati wa wikiendi ya Pasaka.”

Avery A., umri miaka 17, Nevada, Marekani

“Nilisoma Injili na historia ya maisha ya Yesu! Ni furaha kubwa kujifunza kumhusu Yeye wakati wa Pasaka.”

Esteban A., umri miaka 15, San José, Costa Rica

“Katika French Polynesia, tulikuwa na burudani ya vijana wa imani zote ya Pasaka. Kupitia dhoruba na mawimbi, Bwana aliifanya kuwa usiku wa miujiza, shangwe, na umoja.”

Tehina C.T., umri miaka 24, Tupua‘i, French Polynesia

“Mwaka huu nilifokasi kwenye kujifunza kile Kristo alifanya wakati wa Wiki Takatifu.”

Maddysen R., miaka 18, Utah, Marekani