Huitajiki Kuwa Mbobezi
Mwenye “kipaji” au la, kila mtu anaweza kupata mwongozo wa kiungu.
Vielelezo na Getty Images
Wengi wetu tumeweza kuwa na uzoefu wa kukutana na sanaa kubwa au burudani na kufikiria: “Natamani ningeweza kufanya hivyo, lakini sina vipaji vya kutosha.”
Nyingi ya kazi zako pendwa kwa hakika zilifanywa na watu wenye vipaji vingi vya asili. Lakini utashangaa ni mara nyingi kiasi gani ilikuwa ni mtu wa kawaida tu aliyekuwa na wazo la kuvutia.
“Let Easter Anthems Ring,” mojawapo ya nyimbo mpya ambazo Kanisa limezitoa hivi karibuni, uliandikwa na Mtakatifu wa Siku za Mwisho aitwaye Larry A. Hiller. Alikuwa mwandishi wa kitaaluma na mhariri (mstaafu sasa), lakini sio mwandishi wa nyimbo. Hakuwa mwimbaji mzuri au mwanamuziki.
Alikuwa mtu tu fulani ambaye alipenda muziki na alikuwa na wazo lenye mwongozo wa kiungu.
Wakati akihudumu kama mkurugenzi wa kwaya wa kata miaka mingi iliyopita, Kaka Hiller alijaribu mkono wake katika kuandika maneno mapya kwa ajili ya wimbo wa zamani aliougundua. Alifurahia uzoefu huo na kumuuliza rafiki aliyefanya kazi Kanisani kama alijua nyimbo zingine zozote ambazo zilihitaji maneno mapya. Alimwonyesha kwenye tuni ya wimbo uliotungwa katika miaka ya 1800.
Kaka Hiller alisema, “Nilikaa chini na muziki huo na maneno yalikuja akilini mwangu mara moja: ‘Inukeni, enyi Watakatifu, shangilieni.’ Na kutoka hapo nilihisi maandishi ya jumla na kile kilicho hitajika kuwa—wimbo wa kufurahia kuhusu Mwokozi.”
Wimbo huo ulichapishwa katika jarida la Ensign mwaka 2012. Ulikuwa na beti nne na ulikuwa juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. “Ulikuwa na fokasi imara juu ya ‘utawaona wapendwa wako tena; kuna ufufuko,’” Kaka Hiller alisema. Wakati Kanisa lilipotoa wito wa nyimbo mpya za dini, Kaka Hiller aliombwa kufokasi tena maneno yake mahususi kwenye Pasaka.
Baada ya kubadilisha mashairi mengi—ingawa mstari wa ufunguzi, “Inukeni, enyi Watakatifu, shangilieni,” ulibaki—Kaka Hiller sasa alikuwa na wimbo wa beti tatu unaoitwa “Let Easter Anthems Ring.” Mnaweza kuuimba katika mkutano wa sakramenti msimu huu wa Pasaka!
Je, Kaka Hiller alihisi msukumo wakati alipoandika maneno haya?
“Inanyenyekeza kusema hivyo,” alisema. “Lakini ndiyo. Kumekuwa na nyakati ambapo nilihisi mtiririko wa maneno ukinijia akilini mwangu. Inafurahisha na kwa ukimya inaleta shangwe. Na mara nyingi ninaweza kuhisi mwangwi wa shangwe ile wakati niliposoma tena kitu ambacho hasa kilinisisimua wakati huo. Hiyo peke yake hurudisha hisia hizo za ushuhuda. Ni kama vile kupitia upya uzoefu ule.”
Watu labda watapenda wimbo, lakini inaonekana kama mtu aliyepata zaidi ya hiyo alikuwa (drumroll) … yule aliyeuandika! Kutumia vipaji vyetu na mawazo yetu yenye mwongozo siyo tu huwabariki wengine—hutubariki sisi, pia.