Rafiki
Kama Mtoto Mdogo
Januari 2026 Rafiki


“Kama Mtoto Mdogo,” Rafiki, Januari 2026, 16.

Kama Mtoto Mdogo

Imetoholewa kutoka “Kama Mtoto Mdogo,” Liahona, Mei 2025, 7–9.

Katika mkutano mkuu mwaka jana, Rais Holland alisimulia hadithi kutoka kwenye maisha ya Mwokozi. Siku moja Mitume Wake walikuwa wakibishana kuhusu nani alikuwa mkuu. Kisha Yesu akamwita mtoto mdogo aje Kwake. Yeye alisema “Ye yote … ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni” [Mathayo 18:4]. Rais Holland alisema kwamba watoto wachanga na watoto ni ukumbusho wa ufalme wa Mungu.

Jifunze

Je, inamaanisha nini kuwa mnyenyekevu?

  1. Kushinda katika kila kitu

  2. Kumgeukia Baba wa Mbinguni na wengine kwa ajili ya msaada

  3. Kuwafikiria wengine kabla wewe mwenyewe

  4. Yote b na c

Mosia 3:19 ni andiko lingine ambalo linafundisha kwamba tunapaswa kuwa kama mtoto. Ni ipi kati ya sifa zifuatazo haijajumuishwa katika mstari huu?

  1. Mdadisi

  2. Kujawa na upendo

  3. Mvumilivu

  4. Mnyenyekevu

Ukurasa wa PDF