“Kumfuata Yesu huko Ufilipino,” Rafiki, Januari 2026, 10–11.
Kumfuata Yesu huko Ufilipino
Kutana na Adam
Adam anamfuata Yesu Kristo kwa kuwasaidia wengine. Wakati mmoja shuleni, mwanafunzi mwenzake hakuwa na chakula chochote cha mchana. Adam aliamua kushiriki naye chakula cha mchana. Anasema, “Nilihisi furaha kwa sababu nilipata kumsaidia mtu, kama Yesu alivyofanya.”
Adam pia anamfuata Yesu kwa kusali. Hivi karibuni aligombea urais wa baraza lake la wanafunzi shuleni. Alisali na kumwomba Baba wa Mbinguni amsaidie afurahie matokeo yoyote katika uchaguzi. “Sikushinda, lakini najua Bwana ana mipango mizuri kwa ajili yangu,” Adam anasema.
Kuhusu Adam
Umri: miaka 10
Kutoka: Rizal, Ufilipino
Lugha: Tagalogi, Kiingereza
Lengo: Kuwa daktari mpasuaji ili aweze kuwasaidia watu
Uraibu: Kukaa na marafiki na kucheza badmintoni
Familia: Adam, Mama, Baba, dada wawili wakubwa na kaka wawili wakubwa.
Mambo Ayapendayo Adam
Hadithi ya Maandiko: Wakati Yesu Kristo alipofufuka, kwa sababu inamaanisha kwamba tunaweza kuishi tena pia
Sikukuu: Krismasi
Chakula: Nilaga (mchuzi wa nyama ya nguruwe, boki choyi, na viazi)