Rafiki
Ubatizo ni Zawadi ya Shangwe
Januari 2026 Rafiki


“Ubatizo Ni Zawadi ya Shangwe,” Rafiki, Januari 2026, 2–3.

Kutoka kwa Urais wa Msingi

Ubatizo ni Zawadi ya Shangwe

Picha ya mvulana akitoka majini baada ya kubatizwa kwenye kisima

Wakati mmoja nilizungumza na mvulana ambaye alikuwa na wasiwasi kuhusu kubatizwa. Alikuwa na wasiwasi kwamba angewajibika kwa dhambi zake zote.

Nilimwambia kwamba ubatizo ni zawadi ya shangwe, na haihitaji kuogopa. Mara unapobatizwa, Baba wa Mbinguni anaweza kukusaidia zaidi! Rais Nelson alifundisha kwamba wakati unapobatizwa na kufanya agano na Mungu, Yeye kamwe hataacha kukusaidia wewe.* Baba wa Mbinguni anakualika kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili akuongoze wakati unapothibitishwa. Na unapofanya uchaguzi usio sahihi, unaweza kutubu na kusamehewa kwa sababu Mwana wa Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, tayari alilipa gharama ya dhambi zako.

Ni baraka iliyoje kwamba Baba wa Mbinguni anakualika katika umri wa miaka minane kufanya agano na Yeye ili Yeye aweze hata kukubariki zaidi! Shangwe nyingi zinakungoja unapochukua hatua hii kumfuata Yesu Kristo.

Ninapobatizwa, Ninaweza …

Kumbuka ahadi zangu za ubatizo ninapopokea sakramenti.

(3 Nefi 18:6–7)

Kupata Roho Mtakatifu awe nami daima.

(Yohana 6:52; Mafundisho na Maagano 20:77)

Kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo.

(Mafundisho na Maagano 20:37)

Kujichukulia jina la Yesu Kristo juu yangu na kumfuata Yeye kila siku.

(Mosia 5:8)

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Bryan Beach

  • Rais Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022, 6.