“Ninapobatizwa,” Rafiki, Januari 2026, 29.
Ninapobatizwa
Kwa kutafakari
1. Natazama upinde mvua inyeshapo
Na ninatafakari ardhi isafishwavyo.
Maisha yangu na yawe safi kama ardhi.
Niwe mwema na kwa Mungu tena nikaishi.
2. Namfuata Yesu ninapobatizwa
Na ninaporudi kwake ninasamehewa.
Maisha yangu na yawe safi kama ardhi.
Niwe mwema na kwa Mungu tena nikaishi.