“Kwa hiyo Umeshabatizwa. Sasa Nini Kinafuata?” Rafiki, Januari 2026, 36–37.
Kwa hiyo Umeshabatizwa. Sasa Nini Kinafuata?
Je, tayari umeshabatizwa? Hiyo ni vizuri sana! Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanafurahi sana ulifanya uchaguzi huo wa kuwafuata Wao.
Ubatizo ni mojawapo tu ya hatua za kwanza katika safari yako kwenda kwenye uhusiano wa ajabu wa agano na Baba wa Mbinguni na Mwokozi wako. Hapa kuna baadhi ya vitu unavyoweza kuendelea kufanya au kuanza kufanya sasa ambavyo umeshabatizwa.
Msikilize Roho Mtakatifu
Unakumbuka ulipopokea kipawa cha Roho Mtakatifu baada ya ubatizo wako? Sasa Yeye daima anaweza kuwa pamoja nawe unapochagua mema. Roho Mtakatifu mara nyingi huwasiliana nasi kupitia mawazo na hisia. Kumsikiliza Roho Mtakatifu kutakusaidia kufanya chaguzi nzuri na kupata furaha ya kweli.
Fikiria Kuhusu Hili: Ni wakati gani ulihisi Roho Mtakatifu? Inaweza kuwa uzoefu mkubwa au mdogo!
Tubu
Wakati Yesu Kristo alipofanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, Yeye alifanya iwezekane kwetu sote kutubu. Toba inamaanisha kugeuka kutoka kwa chaguzi mbaya na kumgeukia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wanafurahia sana tunapochagua kutubu kwa sababu inatusaidia kuwa karibu na Wao.
Fikiria Kuhusu Hili: Ni kitu gani kimoja unaweza kufanya ambacho kitakusaidia kugeuka ili kuelekea kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
Pokea Sakramenti
Baada ya ubatizo wako, sakramenti ni maalum zaidi. Sasa unapopokea sakramenti, unafanya upya agano ulilofanya wakati wa ubatizo kutii amri na kumfuata Yesu Kristo. Wakati hauweki ahadi hizi kikamilifu, sakramenti ni ukumbusho wa kila wiki kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kutubu na kusamehewa.
Fikiria Kuhusu Hili: Ni njia gani moja unayoweza kuifanya sakramenti kuwa maalumu wiki hii?
Jiandae kwa ajili ya Hekalu
Hekalu ni nyumba takatifu ya Mungu. Mwaka unaofikisha miaka 12, unaweza kwenda hekaluni na kuwasaidia wengine kwa kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu. Baadaye, unaweza kufanya maagano zaidi yako mwenyewe na Baba wa Mbinguni. Kile unachojifunza hekaluni kitakusaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo!
Fikiria Kuhusu Hili: Ni kitu gani kimoja unachoweza kufanya sasa ili kujiandaa kwenda hekaluni?
Vielelezo na Alyssa Petersen