“Muujiza Mlangoni,” Rafiki, Januari 2026, 18–19.
Muujiza Mlangoni
Je, mama yake Gracie angekuwa SAWA?
Hadithi ya kweli kutoka Marekani.
Gracie alimaliza kipande cha mwisho cha chapati maji, kuweka vyombo vyake katika sinki, na kutwaa mkoba wake wa mgongoni.
“Muda wa sala ya familia,” Baba alisema.
Kila mtu alipiga magoti sebuleni. Kaka pacha wa Gracie, George, alisema sala. “Tafadhali tusaidie kuwa na siku nzuri shuleni,” alisema. “Na tafadhali mbariki Mama kwamba atakuwa SAWA. Tafadhali wabariki madaktari kujua jinsi ya kumsaidia.”
Mama yake Gracie alikuwa na uvimbe wa ubongo. Angehitaji kufanyiwa upasuaji. Madaktari walikuwa na matumaini kwamba kila kitu kingekuwa SAWA, lakini hawakuweza kujua kwa uhakika.
Baada ya sala, Mama alimpa kila mmoja kumbatio. “Ninakwenda tena kwa daktari leo. Natumaini tunaweza kupata majibu zaidi.”
Vipi kama Mama atakufa na siwezi kuzungumza naye tena? Gracie alishangaa. Aliogopa sana. Hangeweza kufikiria kutoweza kumkumbatia Mama au kumuona baada ya shule.
Siku hiyo, Gracie alikwenda darasani, mapumziko, na chakula cha mchana kama kawaida. Lakini aliendelea kumfikiria Mama. Alipohisi woga, alifikiria kuhusu wimbo alioupenda wa Msingi. Familia zinaweza kuwa pamoja milele kupitia mpango wa Baba wa Mbinguni, aliimba akilini mwake.
Walipofika nyumbani kutoka shuleni, Gracie na George walikimbia ndani na kumpa Mama kumbatio kubwa. “Je, miadi yako ilikwendaje?” Gracie aliuliza.
“Ilienda vizuri,” Mama alisema. “Bado hatujui mengi. Nina miadi michache zaidi wiki ijayo kabla ya upasuaji.”
Gracie alifurahi kumwona mama yake. Lakini bado alikuwa na wasiwasi.
Siku chache baadaye, kengele ya mlango ililia. Wakati Mama alipofungua mlango, Gracie alimsikia akiimba.
Alisimama pamoja na Mama mlangoni na kutazama umati wa marafiki wa familia kutoka kanisani na shuleni. Walikuwa wakiimba nyimbo za Msingi. “Tumekuwa tukikufikiria na tulitaka kuleta faraja,” mmoja wao alisema. Kisha walianza kuimba tena.
George alikuja mlangoni pia. Alimgeukia Gracie. “Hebu tuimbe pamoja nao!”
Gracie na George walitwaa makoti yao na kukimbia nje ili kujiunga na wengine. Waliimba kwa sauti kadri vile wangeweza:
Gracie alimwona Mama akifuta machozi. Dada yake mdogo, Rosie, alishikilia miguu ya Mama na akasikiliza pia.
Hisia ya amani ilisambaa juu ya Gracie. Alikuwa bado na wasiwasi kuhusu Mama. Lakini alijua kwamba Yesu Kristo aliwapenda. Yeye alikuwa Mungu wa miujiza. Na kwa namna fulani, Gracie alijua ,mambo yangekuwa SAWA.
Vielelezo na Bethany Stancliffe