Rafiki
Adamu na Hawa
Januari 2026 Rafiki


“Adamu na Hawa,” Rafiki, Januari 2026, 46–48.

Njoo, Unifuate

Adamu na Hawa

Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni pamoja na wanyama

Adamu na Hawa walikuwa watoto wa kwanza wa Baba wa Mbinguni kuishi duniani. Waliishi katika Bustani ya Edeni.

Mti wa uzima

Mungu aliwaacha wale matunda ya kila mti isipokuwa mmoja. Ikiwa wangekula kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya, wangepaswa kuondoka bustanini na hatimaye wangekufa. Lakini Shetani aliwadanganya. Alisema ikiwa wangekula tunda, wangejua mema na mabaya lakini hawangekufa.

Hawa akitwaa tunda kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Hawa alichagua kula tunda.

Mikono ya Hawa ikipitisha tunda hadi mikononi mwa Adamu

Kisha alimpa Adamu sehemu ya tunda. Adamu pia alichagua kula tunda.

Adamu na Hawa wakijificha katika vichaka wakati Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanapotokea

Mungu na Yesu Kristo waliwatembelea, lakini Adamu na Hawa waliogopa na walijificha. Mungu aliuliza kama walikuwa wamekula tunda kutoka kwenye ule mti.

Adamu na Hawa wakiwa wamevalia makoti ya ngozi na kuondoka kutoka kwenye Bustani ya Edeni

Adamu na Hawa walisema kwamba walikula tunda. Sasa iliwabidi kuondoka kutoka kwenye Bustani ya Edeni. Lakini Mungu alikuwa na mpango kwa ajili yao. Sasa walijua mema na mabaya na wangeweza kupata watoto

Adamu na Hawa pamoja na familia yao

Adamu na Hawa waliahidi kutii amri za Mungu. Walijifunza zaidi kuhusu Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Walihisi shangwe kubwa kwa sababu Yeye angeisaidia familia yao kurudi kwa Mungu.