Rafiki
Margo and Paulo
Januari 2026 Rafiki


“Margo na Paulo,” Rafiki, Januari 2026, 26.

Margo & Paulo

Uchaguzi wa Mpatanishi

Kwa nini ninyi wawili mko kimya sana? Kwa kawaida ninyi ni wachangamfu sana!

Walikuwa na mapigano kuhusu kusafisha chumba chao.

Mapema …

Vema! Sara Magamba Nyinyirika itagawanya chumba chetu. Ukimruka, yeye ATAKUNG’ATA!

Sitaki kuja upande wako hata hivyo! Daima ni mchafu!

Je, kweli mtapuuzana usiku kucha?

Hii sio njia ya ukarimu sana kwa kaka na dada kutendeana.

Hata sitaki kuwa kaka yake tena!

Sikukusudia hilo. Nilikuwa tu nimekasirika sana! Natamani ningeweza kugeuza mambo.

Huwezi kumeza maneno yako. Lakini bado unaweza kujaribu kufanya mambo kuwa sahihi.

Unamaanisha ninaweza kutubu. Sawa!

Sawa! Yesu Kristo alilipia dhambi kwa ajili yako ili uweze daima kutubu na kujaribu tena.

Ninajua kile ninachohitaji kufanya. Na nadhani niko tayari sasa.

Baadaye …

Margo” Naomba kuingia ndani?

Wee, ulifanya haya yote?

Kwa usaidizi wa Mama. Samahani daima ninafanya kiwe kichafu. Ninaahidi kufanya vizuri!

Ninasikitika nilikufokea na kukufanya mwenye huzuni.

Nimekusamehe. Labda hatuhitaji Sara Magamba Nyinyirika kugawanya chumba chetu baada ya yote?

Ninafurahi sana kuwa wewe ni dada yangu.

Mimi pia.

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Katie McDee