“‘Punde Nitakuwa na Umri wa Miaka Nane,’” Rafiki, Januari 2026, 20–21.
“Punde Nitakuwa na Umri wa Miaka Nane”
Wakati binti yangu alipokuwa na umri wa miaka sita, tulijaribu sana iwezekanavyo ili atazame ubatizo wa watoto wengine. Baada ya kila ubatizo, tulizungumza naye kuhusu kile kilichotokea. Tulimsaidia kuelewa kwamba atakapokuwa mkubwa vya kutosha kubatizwa, angeweza kuhukumu mema na mabaya. Baada ya kila ubatizo, angesema, “Punde nitakuwa na umri wa miaka nane, nami nitabatizwa pia.”
Mwishowe binti yangu akawa na umri wa miaka nane. Alibatizwa na kuthibitishwa. Sasa alipata kipawa cha Roho Mtakatifu. Tulimwambia kwamba mojawapo ya njia bora za kubaki na Roho Mtakatifu pamoja naye ilikuwa ni kupokea sakramenti.
Tunapopokea sakramenti, sisi tunaahidi daima kumkumbuka Yesu Kristo. Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya mambo Yesu aliyofundisha na kukukumbusha kile unachojifunza kumhusu Yeye nyumbani na katika Msingi. Roho Mtakatifu huongea kwa sauti ndogo, tulivu na atakusaidia kuelewa kile kilicho sahihi na kile kisicho sahihi.
Sasa binti yangu anapenda sana sakramenti! Nawe pia unaweza kupenda. Unapopokea sakramenti kila wiki na kumkumbuka Yesu Kristo, utamhisi Roho Mtakatifu zaidi, na Yeye ataendelea kukuongoza. Utaweza daima kumkumbuka Yesu Kristo.
Hatua za Agano
Paka rangi kila mandhari ili kufuatilia wakati binti wa Mzee Ojediran anapojiandaa kufanya na kushika agano lake la ubatizo.
Vielelezo na Samantha Windley