“Salamu kutoka Ufilipino!” Rafiki, Januari 2026, 8–9.
Salamu kutoka Ufilipino!
Ufilipino ni kundi la visiwa katika Bahari ya Pasifiki ya magharibi. Zaidi ya watu milioni 100 wanaishi huko! Lugha rasmi ni Kifilipino na Kiingereza.
Nchi ya Kisiwa
Kuna zaidi ya visiwa 7,640 nchini Ufilipino. Watu wanaishi kwenye visiwa 2,000 kati ya visiwa hivyo.
Chokoleti ya Majira ya Joto
Milima ya Chokoleti iko katika kisiwa cha Bohol. Wakati wa msimu wa kiangazi, milima hii hugeuka kahawia na kuonekana kama milima mikubwa ya chokoleti!
Tai Mkubwa
Tai wa Ufilipino ni ndege wa kitaifa na moja ya tai wakubwa duniani.
Uvuvi wa Mianzi
Watu hufanya uvuvi sana hapa. Njia mojawapo ya kukamata samaki ni kupiga makofi maji kwa kipande kirefu cha mwanzi. Hii huwashtua samaki wakaigia kwenye nyavu zao.
Muda wa Kusherehekea!
Huku Ufilipino tunasherehekea Krismasi kwa miezi minne, kuanzia Septemba. Tunaanza kucheza muziki wa Krismasi na kupamba hadi msimu utakapomalizika mapema mwezi Januari.
Vielelezo na Minna Miná