“Yesu Alibatizwa,” Rafiki, Januari 2026, 6.
Yesu Alibatizwa
Ninaweza Kubatizwa na Kuthibitishwa Pia!
Kubatizwa ni hatua ya kwanza tunayochukua kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo! Chora picha ya siku yako ya ubatizo, iwe tayari imeshatokea au unaitazamia.
Kwa nini ubatizo ni muhimu kwako?
Kwa nini ni muhimu kwa Yesu?
Kujaza Kisima cha Ubatizo
Tunaweza kumfuata Yesu Kristo kwa kubatizwa. Tunapobatizwa na kuthibitishwa, mambo mawili muhimu hutokea: tunafanya agano na Baba wa Mbinguni, na tunapokea zawadi maalum! Fanya shughuli hii hapo chini ili kujifunza zaidi. Anza chini ya kisima cha ubatizo na ujibu swali. Kisha paka rangi maji kwa kiwango hicho na uendelee hadi kiwango kinachofuata.
-
Unahitaji kuwa na umri wa miaka mingapi ili kubatizwa? (Mafundisho na Maagano 68:27)
-
Ni kiasi gani cha mwili wako kinakwenda chini ya maji? (3 Nefi 11:26)
-
Je, unamuahidi nini Baba wa Mbinguni? Mosia 18:10; Mafundisho na Maagano 20:37
-
Ni zawadi gani unapokea baada ya kubatizwa? (Mafundisho na Maagano 33:15)
-
Unaweza kufanya nini kila wiki ili kukumbuka agano ulilofanya wakati wa ubatizo? (Mafundisho na Maagano 27:2)
Kielelezo na Kelly Smith