Ni Wapi Unaweza Kupata Nguvu Wakati Unapohisi Kukataliwa?
Miaka michache iliyopita, nilishiriki katika shughuli pamoja na vijana wengine na wamisionari kadhaa. Lengo letu lilikuwa kuwaalika watu kuja na kuhudhuria mkutano maalumu wa sakramenti.
Nilifurahi kujiweka katika viatu vya wamisionari wetu. Tulifanikiwa kusambaza mialiko yetu kwa watu wachache tuliokutana nao. Ilipofika muda wa kutoa kadi ya mwisho, Roho alinisukuma kwenda kwa mtu mahususi. Lakini mtu yule alijibu vibaya mwaliko wetu na kutufukuza.
Ilinifanya nihuzunike kuona mtu huyu akikataa upendo wa Mwokozi wetu. Ninajua kwamba watu wengi wanakataa mwaliko wa Kristo wa kuja Kwake. Lakini pia ninajua kwamba kwa kutoa mwaliko huu tu, tunapanda mbegu katika mioyo ya watu. Uzoefu huu uliimarisha ushuhuda wangu ingawa mwaliko wangu ulikataliwa. Ninajua kwamba tukiwa na Kristo, chochote kinawezekana, na nimeendelea kujitayarisha kuhudumu misioni na kuwaleta wengine Kwake na kwa Baba yetu wa Mbinguni.
Jalil T., umri miaka 17, Jimbo la Kusini, New Caledonia
Anafurahia muziki, soka, na kupiga kambi na kutembea pamoja na familia yake.