2025
Siku mbaya Iligeuka kuwa Nzuri
Machi 2025


Siku mbaya Iligeuka kuwa Nzuri

msichana akitazama saa yake ya kengele

Ah, hapana! Nilipitiwa na usingizi, na nina mtihani mkubwa leo!

msichana akisimamisha teksi ya pikipiki

Wewe! Wewe! Ninahitaji usafiri kwenda shuleni!

Twende basi!

kijana juu ya teksi ya pikipiki

Kweli?

msichana na mvulana shuleni

Leo imekuwa siku MBAYA SANA, na hata mchana haujafika!

Mara ya mwisho nilipokuwa na siku kama hiyo, nilisali. Matatizo yangu hayakuondoka, lakini nilihisi vizuri zaidi.

msichana akisali

Baba wa Mbinguni, tafadhali nisaidie. Tafadhali igeuze siku hii.

wasichana wawili shuleni

Camila! Je, unaweza kuja nyumbani kwetu? Ninahitaji unifundishe jinsi ya kuchora kwa ajili ya mradi wangu wa shule! Ninayo aiskrimu pia.

Hakika, Emi, ningependa kufanya hivyo.

wasichana wawili wakichora na kula aiskrimu

Nadhani siku hii isiyo nzuri iligeuka kuwa nzuri sana baada ya yote.