Njoo, Unifuate
Hazina Zilizofichika
Jizatiti katika maandiko na utapata aina zote za vitu.
Ufunuo wa siku za leo unafafanua maandiko.
Mafundisho na Maagano 19 inaelezea mambo mawili kuhusu Mwokozi.
Luka anasema jasho la Bwana katika Bustani ya Gethsemane “lilikuwa kama matone makubwa ya damu” (Luka 22:44). “Kama ilivyokuwa” inaonyesha kwamba hiyo ni tamathali tu ya semi.
Yesu analifafanua hili. Anasema mateso Yake yalimfanya “kutokwa na damu kwenye kila kinyweleo” (Mafundisho na Maagano 19:18). Hakuna sitiari. Uchungu wake ulikuwa mkubwa sana hakika alitokwa na jasho la damu.
Kwingineko, maandiko yanatumia vifungu vya maneno kama “mateso yasiyo na mwisho” na “adhabu ya milele.” Alma Mdogo anasema “aliteswa kwa mateso ya milele” (Alma 36:12). Lakini mateso yake yalidumu kwa siku tatu tu (ona Alma 36:16). Ni kwa jinsi gani hiyo ni “ya milele”?
Tena, Yesu anafafanua. Kwa kuwa Baba wa Mbinguni na Yesu ni wa milele na hawana mwisho, adhabu yoyote Wanayoitoa ni, kwa ufafanuzi, adhabu ya “milele” au “isiyo na mwisho” bila kujali muda ( ona Mafundisho na Maagano 19:6–12). Ni mateso ya wana wa upotevu tu yatadumu milele (ona Mafundisho na Maagano 76:30–38).
Ubatizo mmoja unatosha—lakini unahitaji mamlaka.
Waongofu yamkini mara nyingi huwauliza wamisionari: Itakuwaje kama tayari nimebatizwa katika kanisa lingine? Je, ninahitaji kubatizwa tena?
Mafundisho na Maagano inaeleza kwamba bila ukuhani— mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu—“hata mtu akibatizwa mara mia haitamfaa chochote” (Mafundisho na Maagano 22:2).
Hivyo jibu kimsingi ni: “Ubatizo wako wa awali ulikuwa tendo la haki kulingana na kile ulichokijua wakati huo. Sasa unajua zaidi, na Bwana anakutaka utende kulingana na ufahamu huo.”
Hakuna mtu aliye mzuri katika kila kitu. Na hivyo ni SAWA.
Nabii Joseph Smith hakuwa mzuri katika biashara au uchumi. Kwa maneno ya kidunia, hakuwa na mafanikio.
Bwana alimwambia ingekuwa hivyo: “Katika kazi za kimwili wewe hutakuwa na nguvu, kwani huo siyo wito wako” (Mafundisho na Maagano 24:9).
Utakuwa na marafiki na wanadarasa wenzako ambao wanaenda kwenye vyuo vikuu bora kuliko wewe , wanapata kazi nzuri zaidi kuliko wewe, na wamepata mafanikio zaidi ya kidunia kuliko wewe.
Kwa hiyo?
Maisha siyo mashindano. Unapaswa kujaribu kwa uwezo wako wote, bila shaka. Lakini usiwe na hofu kama unaona watu wengine wakikupita kwenye njia ya maisha. Huenda wasiwe wanaelekea mwisho huo huo wa safari uendayo wewe! Endelea kufanya kile ambacho Bwana anataka wewe ufanye —“wito” wako—na usihofu kuhusu mipango Yake kwa mtu mwingine yeyote.
Nyumba ya Mungu ni nyumba ya utaratibu.
Mwokozi mara nyingi alimkumbusha Nabii Joseph Smith kwamba kila kitu lazima kifanyike “katika utaratibu” (ona Mafundisho na Maagano 20:68; 28:13; 58:55; 107:84). Unahitaji sheria ama sivyo kuna machafuko.
Lakini hiyo haimaanishi hakuna kamwe njia yoyote tofauti. Kwa mfano, Bwana alimwambia Joseph Smith kwamba “si muhimu ni nini utakacho kunywa au utakachokula wakati unapopokea sakramenti”—ili mradi kwamba unafanya hayo kwa ukumbusho wa mateso Na Upatanisho Wake (Mafundisho na Maagano 27:2).
Linapokuja suala la kuongoza Kanisa, hata hivyo, hakuna matendo tofauti. Mtu mmoja tu kwa wakati mmoja anaweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa: wa kwanza akiwa Joseph Smith (ona Mafundisho na Maagano 28:2); kisha yeyote ambaye Bwana alimteua “baada yake” (Mafundisho na Maagano 28:7)—Brigham Young, John Taylor, na kadhalika mpaka kwa nabii wa leo.
Viongozi wengine wa Kanisa wenye mwongozo wa kiungu wanaweza kufundisha, kushauri, na kutoa ushauri ( ona Mafundisho na Maagano 28:4–5). Lakini ni Rais wa Kanisa pekee anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Mungu kwa mambo yanayolihusu Kanisa zima.