Unganika
Maja C.
16, Drava, Slovenia
Picha na Christina Smith
Mama na baba yangu walitengana nilipokuwa na umri wa miaka miwili na nusu. Ningeenda kumtembelea baba yangu kila mwezi, na nilipokuwa mdogo, hii ilikuwa burudani sana. Lakini nilipokuwa mkubwa, tulikuwa na kutoelewana mara kadhaa na mambo yalikuwa mabaya zaidi na zaidi.
Nakumbuka kumlilia mama yangu kwamba sikutaka kumtembelea baba yangu tena. Yeye alisema, “Sali, na kila kitu kitakuwa vema zaidi.” Na nilifanya hivyo.
Mungu alinisaidia mimi na baba yangu. Sasa tuna uhusiano mzuri zaidi. Tunazungumza, na ananiita anapokwenda nchi yake ya nyumbani, Macedonia, ili niweze kuzungumza na familia yangu huko.
Yesu Kristo daima amekuwa nguvu yangu. Nilipokuwa na changamoto kubwa shuleni au nyumbani, Yeye daima alikuwa pale kwa ajili yangu. Daima nilihisi kwamba Alikuwa akinisaidia.
Ninashukuru kwamba mama yangu alinitambulisha Kanisani na kwa Mungu, kwa sababu kwa kweli imetusaidia sana miaka yote. Mungu na Yesu Kristo daima wanatutafuta.