2025
Kushinda Vikwazo vya Sala
Machi 2025


Kushinda Vikwazo vya Sala

Jinsi gani tunaondoa vikwazo vyetu vya kusali?

mvulana akiruka na kusali

Vielelezo na Andrew Bosley na Derek L. Smith

“Sali daima.” Mwokozi anatoa maelekezo haya mara 10 katika Mafundisho na Maagano. Tunaelewa kwamba ni ya mfano—hatuwezi kiuhalisia kuwa kwenye magoti yetu tukisali kila wakati tunapotembea—lakini wakati mwingine ni vigumu hata kusali mara mbili kwa siku! Jinsi Gani tunashinda hivi vikwazo?

Kikwazo: Kusahau

Sisi ni binadamu. Inatokea.

Suluhisho yamkini:

Husisha sala zako na kitu kingine unachofanya kila siku, ili kwamba unapofikiria kimoja, unafikiria na kingine. Kama unajiona unasinzia sana kuwa na sala ya maana wakati unapoamka au kabla ya kulala, unganisha sala zako kwenye ratiba zingine za mchana na usiku ambazo unazifuata kwa makini, kama vile kupiga mswaki meno yako au kunywa dawa. Au weka kengele kwenye simu yako!

Kikwazo: Hakuna cha kuripoti

Kuna nini cha kusema asubuhi wakati yote uliyoyafanya tangu sala yako ya mwisho ni usingizi?

Suluhisho yamkini:

Asubuhi mshukuru Mungu kwa baraka zako, ikijumuisha watu binafsi wanaobariki maisha yako. Waombee watu hao. Mwambie Mungu kile ulichopanga kwa ajili ya leo na uombe mwongozo Wake. Wakati wa usiku, toa ripoti. Mwambie kila kitu kilichotokea wakati wa mchana ambacho una shukrani nacho, ambacho ulijifunza kutokana nacho, au ambacho umeona ni cha kuvutia.

Kikwazo: Hisia Hasi

Pengine unahisi kutostahili kwa sababu ya kitu ulichofanya—au unachofikiria kukifanya. Pengine umemkasirikia Mungu kwa kitu fulani. Labda hauko tu katika hali nzuri.

Suluhisho: Omba hivyo hivyo

Popote pale zilipo hisia zako, Mungu anaweza kuzifyonza. Hakuna yeyote, yeyote yule, “asiyestahili” kusali, na ni ibilisi ambaye anataka ufikirie hivyo (ona 2 Nefi 32:8). Baba yako angependa kusikia sala yako isiyo kamilifu, isiyokamilika—sala ambapo unatoa hoja ya kutotaja Jambo Kubwa ambalo hujisikii kulizungumzia bado—kuliko kutosikia kabisa kutoka kwako.