Karibu kwenye Toleo Hili
Msaada kwa ajili ya Siku Ngumu
Maisha hayaendi kila mara jinsi tunavyotumaini itakuwa. Sisi sote tunapenda siku zilizojawa na sherehe na shangwe, lakini baadhi ya siku zimejawa na kuvunjika moyo. Katika toleo hili, utapata msaada kwa ajili ya siku hizo (ona ukurasa wa 8, 14, na 22).
Mojawapo ya maandiko niyapendayo yana kipande cha ushauri na ahadi kwa ajili ya siku ngumu. Yanasomeka, “Kuwa mvumilivu katika mateso, kwani utapata mengi; lakini utayastahimili, kwani, lo, Mimi nipo pamoja nawe, hata mwisho wa siku zako” (Mafundisho na Maagano 24:8). Ushauri ni kuvumilia.
Katika mzizi wake, kuvumilia humaanisha kubaki imara ndani ya majaribu. Hiyo inaweza kuwa vigumu kufanya, ndiyo sababu ninaipenda ahadi kwamba “Mimi nipo pamoja nawe.” Ahadi hiyo inamaanisha kuwa hatuhitaji kupitia siku ngumu peke yetu. Bwana atatusaidia tubaki imara ndani ya majaribu.
Bila kujali kinachotokea katika maisha yetu, njia bora ya kuunganika na Baba ni kusali. Hakika yupo. Yeye atasikia na kujibu sala zetu. Mungu husikia na kuzungumza na watoto Wake katika siku nzuri na siku mbaya (ona ukurasa wa 2). Yeye ameahidi kutembea pamoja nasi.
Kwa upendo,
Emily Belle Freeman
Rais Mkuu wa Wasichana