“Kanisa huko Mongolia,” Liahona, Sept. 2025.
Kanisa huko Mongolia
Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho limekua kwa kasi huko Mongolia tangu wamisionari waandamizi wanandoa walipowasili kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Waongofu wa kwanza katika Mongolia walibatizwa mwaka 1993, na tawi la kwanza lilianzishwa mwaka huo huo. Mnamo 1995, misheni ya kwanza ilianzishwa. Leo, Kanisa huko Mongolia lina:
-
Waumini 12,400 (kwa makadirio)
-
Vigingi 2, kata na matawi 24, na misheni 1
-
Hekalu 1 (kujengwa katika Ulaanbaatar)
Baraka za Kiroho
Munkh-Od Altansukh (juu, kulia) kutoka Kigingi cha Ulaanbaatar East anasema, “Ninapata uzoefu wa kiroho wa thamani kupitia vitendo mbalimbali kama kujifunza maandiko, huduma kwa wengine, na ibada ya hekaluni. Ninajua kwamba vitu vidogo na rahisi vya injili vinavyotekelezwa mara kwa mara vitatusaidia kuendelea kuelekea kuinuliwa kama familia.”