“Bwana ameiteua familia kuwa kitengo cha msingi cha Kanisa na jamii.” Familia zinaweza kuwa na mume na mke pamoja na watoto, na zinaweza pia kuwa mtu mmoja, mzazi mmoja na watoto, au mume na mke bila watoto. Na wakati mwingine familia hizi zinaweza kuwajumuisha ndugu wengine. Bila kujali hali yetu ya kindoa au hali ya mtu binafsi, kila mmoja wetu ni wa sehemu ya familia ya Mungu, kila mmoja wetu ni mshiriki wa familia duniani, na sisi kila mmoja wetu anajitayarisha kuwa wazazi wa milele.
Kwa milenia, manabii na mitume wametangaza utakatifu wa familia na kuonya juu ya majanga yatakayowapata watu binafsi, mataifa na ulimwengu kama familia hazitahifadhiwa na kulindwa. Haya ni baadhi ya maneno ya kuvutia kutoka kwa manabii na mitume kuhusu familia na umuhimu wa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”
“Muhimu kwa mpango wa Mungu ni familia. Kwa kweli, lengo la mpango huu ni kuinuliwa kwa familia. Dunia iliumbwa ili kwamba sisi kama watoto wa kiroho wa Baba yetu wa Mbinguni tuweze kuja duniani na kupata miili ya nyama na mifupa. Tuko hapa ili kujaribiwa na kupimwa [ona Ibrahimu 3:24–25 ]. Tuko hapa ili ‘kuchagua uhuru na uzima wa milele … au kuchagua utumwa na kifo’ [2 Nefi 2:27 ]. Na bora zaidi ya yote, tunaruhusiwa kupendana katika mapenzi, kufunga ndoa, na kuwaalika watoto katika familia zetu (Faith and Families , Ensign , Mar. 2007, 39).
Wale ambao hawauelewi kikamilifu mpango wa upendo wa Baba kwa ajili ya watoto Wake wanaweza kufikiria tangazo hili la familia kama kauli ya sera ambazo zinaweza kubadilishwa. Kinyume chake, tunathibitisha kwamba tangazo la familia, lililopatikana kutokana na mafundisho yasiyobadilika, linafafanua aina ya uhusiano wa familia ambapo sehemu muhimu sana ya maendeleo yetu ya milele inaweza kutokea” (“Upendo wa Kiungu katika Mpango wa Baba ,” Liahona , Mei 2022, 103).
Maisha ya Familia katika Maisha ya Duniani Hututayarisha Kwa Ajili ya Milele
Rais Henry B. Eyring
Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza
“Kitengo cha familia sio tu msingi kwa jamii na Kanisa bali pia kwa tumaini letu kwa ajili uzima wa milele. Tunaanza kufanya mazoezi katika familia, kitengo kidogo, kile kitakachoenea kwa Kanisa na kwa jamii tunayoishi katika ulimwengu huu na kile ambacho hapo ndipo kitakuwa kile tunachofanya katika familia zilizounganishwa pamoja milele kwa njia ya maagano na uaminifu” (“The Family ” [Brigham Young University devotional, Nov. 5, 1995], 8, speeches.byu.edu).
“Uhusiano wa kimapenzi umehifadhiwa kwa ajili ya wanandoa kwa sababu ni ishara kuu ya muungano kamili, muungano uliotawazwa na kufafanuliwa na Mungu. Kutokea kwenye Bustani ya Edeni na kuendelea, ndoa ilikusudiwa kumaanisha muungano kamili wa mwanaume na mwanamke—mioyo yao, matumaini, maisha, upendo, familia, siku zao zijazo, kila kitu. … Huu ni muungano mkamilifu wa jinsi hiyo kwamba tunatumia neno kuunganisha ili kufikisha ahadi yake ya milele” (“Personal Purity ,” Ensign , Nov. 1998, 76; Liahona , Jan. 1999, 91).
Upendo wa mzazi kwa mtoto ni mojawapo ya kani zenye nguvu zaidi katika ulimwengu. Ni mojawapo ya mambo machache hapa duniani ambayo hakika yanaweza kuwa ya milele.
“Sasa, labda unahisi kwamba uhusiano wako na mtoto wako haufai. Hapo ndipo nguvu za Mwokozi zinapoingia. Yeye huponya wagonjwa, na anaweza kuponya uhusiano. Yeye huzidisha mkate na samaki, na anaweza kuzidisha upendo na furaha katika nyumba yako” (“Yesu Kristo ni Nguvu za Wazazi ,” Liahona , Mei 2023, 56).
Imarisha Viungo vya Familia, Hata Kama Baadhi Vinaweza Kuvunjwa
Mzee David A. Bednar
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
“Kwenu [vijana wakubwa] ambao mmepitia maumivu ya moyo ya talaka katika familia yako au mlihisi maumivu ya uaminifu uliokiukwa, tafadhali kumbuka inaanza tena nawe! Kiungo kimoja katika mnyororo wa vizazi vyako yawezekana kimevunjika, lakini viungo vingine viadilifu na kile kinachobaki katika ule mnyororo hata hivyo ni muhimu milele. Unaweza ukaongeza nguvu katika mnyororo wako na pengine hata kusaidia kurejesha vile viungo vilivyovunjika. Kazi hiyo itatimizwa moja baada ya nyingine” (“A Welding Link ” [worldwide devotional for young adults, Sept. 10, 2017], Gospel Library).
“Wanawake na wanaume wana majukumu ya kipekee kama ilivyoonyeshwa katika ‘Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,’ lakini usimamizi wao ni sawa katika thamani na umuhimu. Wana nguvu sawa ya kupokea ufunuo kwa ajili ya familia yao. Wanapofanya kazi pamoja kwa upendo na haki, maamuzi yao yanabarikiwa mbinguni” (“Upendo Mkuu kwa Watoto wa Baba Yetu ,” Liahona , Mei 2019, 79).
Wazazi Wanapaswa Kuwaongoza Watoto kwenye Tumaini katika Kristo
Mzee D. Todd Christofferson
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
“Mungu aliamuru kwamba wanaume na wanawake wanapaswa kuoana na kuzaa watoto, kwa hivyo kuumba, katika ubia na Mungu, miili ya nyama na mifupa ambayo ni muhimu katika majaribio ya duniani na muhimu kwa utukufu wa milele pamoja Naye. Pia aliamuru kwamba wazazi wanapaswa kuanzisha familia na kulea watoto wao katika nuru na ukweli [ona Mafundisho na Maagano 93:36–40 ], na kuwaongoza kwenye matumaini na katika Kristo” (“Kwa Nini Ndoa, Kwa Nini Familia ,” Liahona , Mei 2015, 51).
“Kama tutachukua na kuchagua kile tunachokubali katika tangazo, tunatia wingu mtazamo wetu wa milele, na kuweka umuhimu mkubwa katika uzoefu wetu wa hapa na sasa. Kwa kulitafakari kwa sala tangazo hili kupitia jicho la imani, tunaelewa vyema zaidi jinsi kanuni zinavyounganika vyema, zikisaidiana, zikifunua mpango wa Baba juu ya watoto Wake.(“Familia ,” Liahona , Mei 2019, 35–36).