“Kwa Ajili ya Siku Yetu,” Liahona, Sept. 2025.
Kwa Ajili ya Siku Yetu
Miaka thelathini baada ya tangazo juu ya familia kutambulishwa kwa ulimwengu, kanuni zake takatifu ni za usahihi zaidi na halali kuliko hapo awali.
Rais Gordon B. Hinckley akizungumza na mkusanyiko huko Santiago, Chile
Mnamo Septemba 23, 1995, Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alihutubia mkusanyiko wa akina dada wa Muungano wa Usaidizi na kutambulisha “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Yafuatayo ni baadhi ya maoni yake juu ya tukio hilo:
“Ninaamini kwamba inapaswa kuwa baraka ya kila mtoto kuzaliwa katika nyumba ambayo mtoto huyo anakaribishwa, analelewa, anapendwa, na kubarikiwa na wazazi, baba na mama, ambao wanaishi kwa kuaminiana na kwa watoto wao. …
“Kadiri unavyowalea watoto wako kwa uhakika zaidi katika njia za injili ya Yesu Kristo, kwa upendo na matarajio makubwa, ndivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba kutakuwa na amani katika maisha yao. …
“Pamoja na ujanja mwingi ambao umepitishwa kama ukweli, kwa udanganyifu mwingi kuhusiana na viwango na maadili, kwa mvuto mwingi na vishawishi vya kuchukua doa la ulimwengu pole pole, tumehisi kuonya na kuonya mapema Katika kuendeleza hili sisi Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili sasa tunatoa tangazo kwa Kanisa na kwa ulimwengu kama tamko na uthibitisho wa viwango, mafundisho, na desturi kuhusu familia ambayo manabii, waonaji, na wafunuzi wa kanisa hili wamesema kwa kurudia rudia kote katika historia yake. …
“Tunapendekeza kwa wote kusoma tangazo hili kwa umakini, kwa tafakuri, na kwa sala. Nguvu ya taifa lo lote imekita mizizi ndani ya kuta za nyumba zake. Tunawahimiza watu wetu kila mahali walipo kuimarisha familia zao kulingana na maadili haya yanayoheshimika kwa wakati wote.”