2025
Masomo Niliiyojifunza katika Kumwalika Kristo Aandike Hadithi Yangu
Septemba 2025


“Masomo Niliyojifunza katika Kumwalika Kristo Aandike Hadithi Yangu,” Liahona, Sept. 2025.

Wanawake wa Agano

Masomo Niliyojifunza katika Kumwalika Kristo Aandike Hadithi Yangu

Sote tuna uzoefu tofauti, lakini tukiacha Mungu ashinde katika maisha yetu, tutatimiza kipimo cha uumbaji wetu katika njia ambazo kamwe hatungeweza kufikiria.

mama amembeba mtoto mchanga

Maelezo kutoka Protector by Day and by Night, na Caitlin Connolly, isinakiliwe

Mnamo mwaka 2016—katikati ya karibu miongo mitatu ya ndoa, kuzaa na kulea na kuwapenda wana wetu watatu, kufanya kazi ya sheria kwa muda wote, kuhudumu katika miito ya Kanisa, na kukimu mahitaji ya familia yetu kubwa—mimi pamoja na mume wangu, Doug, tuliitwa kuhudumu kwa miaka mitatu kama viongozi wa misioni huko Arequipa, Peru. Tuliondoka baada tu ya mjukuu wetu wa kwanza kuzaliwa.

Tulirudi nyumbani mwaka 2019 kwa mabinti wajukuu wawili wapya. Wana wetu wawili wakubwa walikuwa wameoa, na mdogo kabisa alikuwa katika mapenzi na punde akaoa. Nilirudi kufanya kazi ya sheria, na wito wangu nilioupendelea ulikuwa kama Mama na Bibi.

Na kisha wito ulikuja kuhudumu kama Rais Mkuu wa Msingi. Simulizi nzuri niliyojiandikia ilikuwa ni kutumia muda pamoja na familia yangu, muongo mwingine nikifanya kazi ya sheria ili kuhakikisha usalama wa kifedha, na kuhudumu katika kata yangu au hekaluni.

Vipi kama ningekwama na simulizi hii ya nzuri?

Ningefurahia kutumia muda mwingi na wajukuu zangu na ningeweza kuwa na uhakika wa usalama wa kifedha. Na ningekosa uzoefu wa kuninyoosha, wa kupekua nafsi na wa kujenga imani. Kupanda mlima? Ndiyo. Unastahili hili? Aha, ndiyo!

Ninatoa ushahidi wangu kwamba “kwa sababu [Mwokozi] anajua uwezekano wetu kikamilifu, Yeye atatupeleka mahali ambapo hatujawahi kujifikiria wenyewe.” Nina uhakika Atakupeleka mahali ambapo hujawahi kufikiria, na huduma yako itakuwa inayonyoosha nafsi. Acha Mungu akuongoze kutembea kando ya mtu anayekuhitaji.

Unaweza kujikuta ukiwafundisha watu wazima kusoma. Au labda kuwahudumia wahamiaji. Pengine utaongoza kikundi cha jumuiya kudumisha na kuweka bustani salama kwa familia. Tunapomruhusu Mungu ashinde, atatupeleka mahali anapotuhitaji sisi na mahali ambapo hatujawahi kufikiria.

Rais Russell M. Nelson alitangaza kwamba sisi “tunapokea zaidi imani kwa kufanya kitu ambacho kinahitaji zaidi imani.”

Ninajua kwamba hilo ni kweli. Kwa sababu kumwacha Mungu ashinde katika maisha yangu, katika kumruhusu Yeye aandike hadithi yangu, imani yangu katika Yesu Kristo imeongezeka.

Basi, je, wewe utamruhusu Yeye ashinde?

Hiyo inaonekana vipi kwa kijana ambaye anatafuta elimu na anataka kuoa na kuwa na familia? Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, ameelezea kwamba uchaguzi si kati ya familia au elimu au kazi. Alisema: “Muda ndio kile tunachopaswa kuchagua, na tunatafuta mwongozo wa kiungu wa Bwana na mafundisho ya watumishi Wake katika kufanya hivyo.”

Katika kuzungumzia mada hii, ningependa kuwa makini kwa wale ambao wana hamu ya dhati na ya kudumu ya kuoa na kuwa na watoto katika maisha haya na ambao hawajaoa wala kuolewa. Ninatambua wengi wanalea kama mzazi peke yao kwa sababu ya kifo au talaka. Ninawajua wanandoa wasio na idadi ambao wameoa au kuolewa na wanatamani watoto na wanateseka kwa ugumba na kuharibika kwa mimba. Ninajua unateseka. Unataka muda ubadilike. Hii sio simulizi uliyojiandikia wewe mwenyewe. Moyo wangu unaumia kwa ajili yenu.

Hadithi ya Kila Mtu Ni Tofauti

Nilitafuta elimu, zote za shahada ya kwanza na digrii ya sheria. Niliolewa katikati ya elimu yangu ya kisheria. Nilipata mwanangu wa kwanza mwaka mmoja baada ya kufaulu uwakili. Nilikuwa na watoto wachanga, na mume wangu na mimi tuliwapenda na kuwalea wakati sote tulipokuwa tukifanya kazi. Ilikuwa ni shughuli nyingi, wakati mwingine ngumu; tulikuwa tumenyooshwa na wakati mwingine tulichoka. Nilimsaidia yeye, na alinisaidia mimi. Familia ilikuwa, na bado ni, kipaumbele chetu cha juu. Mume wangu na mimi tulitafuta mwongozo wa kiungu katika chaguzi hizi na katika ratiba. Ndicho tulichohisi kuvutiwa kufanya. Tulikuwa tunajaribu kumwacha Mungu ashinde.

Kwa mtazamo wa kifedha na kitaaluma, ingekuwa na maana kutokuwa na watoto hadi nitakapokuwa vizuri zaidi katika kazi yangu. Lakini katika kumruhusu Bwana aandike hadithi zetu, wakati mwingine tunafanya vitu ambavyo ulimwengu hauwezi kuvielewa. Nilikimbizana na kubeba ujauzito, kuzaa watoto, kulea watoto, zamu za kuendesha gari, ligi ya besiboli, majukumu ya Kanisa, kuwa mwenza wa msaada, na shughuli zangu za kitaaluma. Ilikuwa mchezo wenye shangwe nisingetaka kuubadilisha. Tulihisi kujiamini katika njia yetu kwa sababu tulikuwa tukimruhusu Mungu ashinde.

Tafadhali msielewe vibaya. Sipendekezi kila mtu afuate njia yangu. Hadithi zetu hazifanani. Ninashiriki yangu kwa sababu ndicho ninachojua. Hata hivyo, kitu kimoja tulichonacho kinachofanana ni motisha yetu: kumwacha Mungu ashinde.

Kuwa mama ni kipaumbele changu cha juu. Ni shangwe yangu kuu. Mungu aliwabariki wazazi wetu wa kwanza na kuwaamuru “zaeni, mkaongezeke, na kuijaza nchi” (Mwanzo 1:28). Amri ya kwanza iliyotolewa kwa Adamu na Hawa “inahusiana na uwezo wao wa uzazi.”

Mwelekeo wangu wa msingi ni kuelekea kwenye umama. Mwelekeo huo haukuwa wa kutofautiana na juhudi yangu ya kutafuta elimu. Tumeamriwa kutafuta kujifunza—baadhi yake huja katika kutafuta elimu. Pia inatokana na uzazi, ambapo tunajifunza kuwa kama mungu tunapokuza sifa za upendo, huruma na subira.

Kumwacha Mungu ashinde hujumuisha kumwalika Yeye ajihusishe katika wakati wa chaguzi zetu.

Nina shukrani za milele kuwa nimepokea maongozi kutoka kwa Bwana na maelekezo kutoka kwa manabii ili kuwasaidia mume wangu na mimi katika muda wa uchaguzi wetu wa kuwaalika watoto katika familia yetu wakati tulipofanya hivyo. Ninashukuru sana nilitenda juu ya misukumo na sikuruhusu ushawishi wa kidunia, urahisi, heshima, au pesa katika njia ya uchaguzi wa kutimiza uwezekano wangu wa kiungu katika kuwazaa na kuwalea watoto.

wanawake wenye watoto na wasio na watoto

Wanawake wenye watoto na wasio na Watoto, na Caitlin Connolly, isinakiliwe

Kipimo cha Uumbaji Wetu

Kama wanaume na wanawake watakoma kuwa na watoto na kuwalea, uzoefu huu wa maisha ya duniani unaisha. Ni muhimu sana, basi, kwamba tusipuuze wala kufutilia mbali jukumu takatifu la uzazi.

Wingi wa takwimu za sayansi ya kijamii zinaonyesha athari mbaya kwa mataifa na ustaarabu unaoondoa kupatikana kwa watoto. Katika sehemu nyingi za ulimwengu, wastani wa idadi ya uzazi hai kwa kila mwanamke ni chache kuliko wawili. Hiyo inamaanisha kwamba hatutafuti mbadala wetu.

Kama viongozi wa Kanisa, tuna wasiwasi kuhusu mitindo ya hivi karibuni katika ndoa na kuzaa mtoto. Nchini Marekani, katika kipindi cha zaidi ya miaka 30 iliyopita, tumeona kiwango cha asilimia nane hadi tisa kikishuka katika raia wale ambao wamewahi kuoa na kuolewa. Takwimu hizi “zinawakilisha tatizo ulimwenguni kote.” Watu wanapokuwa hawaoi au kuolewa, watoto wachache huzaliwa.

Marekani hivi karibuni ilivuka “kizingiti ambapo, watu wazima wenye umri wa miaka 18–55, sasa kuna sehemu kubwa ya watu wazima waseja wasio na watoto kuliko watu wazima waliooana wenye watoto.”

Watoto ni muhimu katika kudumisha ustaarabu. Ni muhimu kwa mpango mtukufu wa furaha. Amri kwa ajili yetu ya kuzaana na kuijaza dunia “bado inatumika.”

kielelezo cha familia imesimama pamoja

Maelezo kutoka Sisi pamoja Nao na Wao pamoja Nasi, na Caitlin Connolly, hayawezi kunakiliwa

Mwache Bwana Aandike Hadithi Yako

Ninajua hamu ya dhati ya mioyo mingi inaweza kuwa kuoa au kuolewa na kulea watoto. Bado wengi ni waseja au wanateseka kwa ugumba. Rafiki yangu mpendwa, ambaye hajawahi kuolewa na kupata watoto wake mwenyewe, amewapenda na kuwatunza wa kwangu. Sio mbadala kwa watoto wake mwenyewe. Ni ushahidi kwamba mwelekeo wake unabaki kuelekea umama.

Mwanangu na binti mkwe wamepitia changamoto ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara. Hamu yao ni ya haki. Wanatafuta kuacha Mungu ashinde katika maisha yao. Kumbuka, tunapoomba kwa imani kumruhusu Yesu Kristo awe mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi yetu, lazima tuwe tayari kucheza simulizi isiyo na raha katika tumaini la kwamba, japo ni chungu, hatimaye itakuwa kuu na ya selestia zaidi kuliko tunavyoweza kufikiria.

Miongoni mwa marafiki zangu wapendwa ni wanandoa wasio na watoto ambao walioana baadaye maishani na kuteseka kwa ugumba. Waliuliza kwa imani kama wanapaswa kuasili watoto. Badala ya mtoto mchanga, walihisi msukumo wa kuwaasili akina dada wanne—wenye umri wa miaka 5 hadi 17. Kabisa, chanya, sio simulizi waliyojiandikia wenyewe. Lakini ee, jinsi gani hadithi ya ajabu ambayo Yeye ameandika pamoja nao.

Bila kujali hali zetu binafsi, sisi sote ni sehemu ya familia ya Mungu, wanafamilia wa kidunia, na kujitayarisha kuwa wazazi wa milele. Baraka za kuinuliwa zilizopatikana kwetu kupitia Mwokozi, Yesu Kristo, zinajumuisha vizazi vijavyo. Na hivyo, iwe tumeunganishwa na kuzaa watoto katika maisha haya au yajayo, lengo letu ni kuinuliwa—ambalo linaweza kuwa letu kama tutafanya na kushika maagano. Tunapoingia katika uhusiano wa agano na Mungu, tunafungwa wima Kwake, na kamwe hatuko peke yetu. Tumebarikiwa kwa “kiasi kikubwa cha upendo na rehema [Zake].”

Kama watu wa agano, tunapanga na kujiandaa kwa ajili ya ndoa na kuwa na watoto na kuwalea. Ni wito mtakatifu ulioje! Tunapenda na kuongoza na kuhudumia na kuwa mzazi ili kuonyesha upendo wetu kwa Mungu na watoto Wake—kwa sababu tunamtaka Yeye ashinde katika maisha yetu.

Ni wakati mtukufu kuwa hai na kufanya maagano katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kuelewa jukumu letu, dhumuni na jukumu katika mpango wa furaha hutuwezesha, huleta hakikisho jipya na shangwe. Kujua kwamba tuna nabii anayeishi anatutayarisha kwa kile kilicho mbele huniletea amani na hata matumaini katikati ya kutokuwa na uhakika. Uhusiano wangu wa agano na Mungu unanipa kujiamini. Kujiamini kwangu kiagano kuko katika Yesu Kristo.

Ninashuhudia kwamba Yeye yu hai, kwamba upendo Wake kwetu unadhihirishwa katika utayari Wake wa kutoa uhai Wake na Upatanisho kwa kila mmoja wetu.

Muhtasari

  1. Camille N. Johnson, “Mwalike Mwokozi Aandike Hadithi Yako,” Liahona, Nov. 2021, 82.

  2. Ona Russell M. Nelson, “The Influence of Women,” (hotuba iliyotolewa katika ibada ya Muungano wa Kina Mama duniani kote, Machi 17, 2024), Gospel Library.

  3. Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 103.

  4. Dallin H. Oaks, katika Face to Face with Elder Oaks and Elder Ballard (worldwide young single adult broadcast, Nov. 19, 2017), Gospel Library.

  5. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Gospel Library.

  6. Ona Dallin H. Oaks, katika “Insights,” Ensign, Mar. 1975, 56–57.

  7. Dallin H. Oaks, “Stand for Truth” (worldwide devotional for young adults, May 21, 2023), Gospel Library.

  8. Ona Dallin H. Oaks, “Stand fo Truth,” Gospel Library.

  9. Chris Bullivant and Brad Wilcox, “Back from the Brink: The Intellectual Tide Is Turning on Marriage and Civil Society,” Deseret News, Apr. 17, 2024, deseret.com.

  10. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Gospel Library.

  11. Ona Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” Liahona, Okt. 2022, 9.

  12. Russell M. Nelson, “Agano Lisilo na Mwisho,” 10.

  13. Ona Ulisses Soares, “Ujasiri wa Agano kupitia Yesu Kristo,” Liahona, Mei 2024, 17–21.