Kwenye Hoja
Sayuni ni nini?
Katika maandiko, neno Sayuni linaweza kumaanisha:
-
Sayuni ni “walio safi moyoni” (Mafundisho na Maagano 97:21).
-
Watu wa Bwana, au Kanisa na vigingi vyake (ona Mafundisho na Maagano 82:14).
-
Mahali maalum ambapo watu wa Bwana wanaishi na kukusanyika, kama vile:
-
Mji wa Henoko (ona Musa 7:18).
-
Mji wa kale wa Yerusalemu (ona 2 Samweli 5:6–7; 1 Wafalme 8:1; 2 Wafalme 9:28).
-
Yerusalemu Mpya—mji utakaojengwa katika siku za mwisho katika Wilaya ya Jackson, Missouri, huko Marekani (ona Mafundisho na Maagano 45:66–67; Makala ya Imani 1:10).
-
Ingawa waumini wa Kanisa leo hawakusanyi mahali pa kati, “tunashiriki katika mradi mkubwa wa kuanzisha Sayuni katika maandalizi ya kurudi kwa Bwana.” Viongozi wetu wametufundisha kuanzisha Sayuni na kuimarisha Kanisa popote tunapoishi. Tunafanya hivi, kwa sehemu, kwa kutafuta kuishi kama watu wa “Sayuni” wanavyoishi. Kwa mfano, katika Musa 7:18 tunajifunza:
-
Wao ni “wa moyo mmoja na wazo moja.”
-
Wanaishi katika haki.
-
na hapakuwa na maskini miongoni mwao.