Njoo, Unifuate
Mafundisho na Maagano 95; 103; 107
Hazina Zilizofichika
Chimba ndani ya maandiko. Ni jambo la thamani.
Bwana kwa Upendo Anatukumbusha Juu ya Amri Ambazo Tumezipuuza.
Katika Mafundisho na Maagano 95, Bwana alivunjwa moyo kidogo na Watakatifu. Awali alikuwa amewaamuru kujenga hekalu (ona Mafundisho na Maagano 88:119)—lakini miezi mitano baadaye, hawakuwa wamefanya chochote kuhusu hilo.
Hiyo inaonekana isiyofikirika leo. Kujenga mahekalu ni fokasi kubwa kwetu! Lakini Bwana hakuwa amefunua mengi kuhusu mahekalu mnamo 1833. Watakatifu hawakuthamini kikamilifu jinsi ambavyo yangekuwa muhimu.
Basi Bwana alifanya nini? Aliingia kwa undani kuhusu kwa nini Aliwataka kujenga hekalu (ona Mafundisho na Maagano 95:8–17). Alifafanua juu ya kile alichosema hapo awali, akitoa umaizi mpya na akisisitiza umuhimu wake.
Dhambi Huleta Kurudiwa, lakini Bwana Bado Anaahidi Baraka.
Mnamo 1834, Watakatifu walikuwa wakijiuliza kwa nini Bwana aliwaacha maadui zao kuwanyanyasa na kuwafukuza kutoka kwenye nchi yao wenyewe. Kupitia Nabii Joseph Smith, Bwana alitoa majibu mawili:
Kwanza, Bwana alisema Wakati mwingine Yeye huwaruhusu waovu kufanya mambo mabaya “ili waweze kujaza kipimo cha uovu wao” (Mafundisho na Maagano 103:3). Alma aliiweka kwa njia hii: “Anakubali kwamba wafanye [vitu vibaya] … kwamba hukumu ambazo atazitumia juu yao katika ghadhabu yake ziwe za haki” (Alma 14:11).
Sababu nyingine Bwana aliyowapa Watakatifu kwa matatizo yao labda ilikuwa vigumu kidogo kuisikia: “Kwamba wale wanaojiita kwa jina langu waweze kurudiwa kwa kipindi kifupi … kwa sababu hawakutii kabisa mawaidha na amri ambazo niliwapa” (Mafundisho na Maagano 103:4).
Hiyo haimaanishi kwamba Mungu aliidhinisha matendo maovu na haramu ya maadui zao. Yeye “hakuwapa uvuvio” magenge ya wahuni kuwashambulia Watakatifu; Aliwaacha watumie haki yao ya kujiamulia na hakuingilia kati kuwazuia.
Lakini Bwana bado aliahidi kwamba kama Watakatifu watatii, “hawatakoma kamwe kushinda” (Mafundisho na Maagano 103:7).
Kwa nini Ukuhani Unaitwa kwa jina la Melkizedeki?
Yawezekana kuwa umejiuliza kwa nini ukuhani wa juu unaitwa kwa jina la Melkizedeki. Bwana alifafanua kupitia kwa Nabii Joseph Smith.
“Kabla ya siku yake [Melkizedeki] uliitwa Ukuhani Mtakatifu, kwa Mfano wa Mwana wa Mungu. Lakini kwa sababu ya heshima au staha kwa jina la huyu Kiumbe Mkuu, ili kuepuka kurudiwa mara kwa mara kwa jina lake, wao, kanisa, katika siku za kale, waliuita ukuhani huo Melkizedeki” (Mafundisho na Maagano 107:3–4).
Fikiria kuhusu ni mara ngapi tunataja “Ukuhani wa Melkizedeki” katika mikutano ya Kanisa na mijadala isiyo rasmi. Sasa fikiria kama, badala ya “Melkizedeki,” tulikuwa tukisema “Mwana wa Mungu” kila wakati. Ingeanza kuonekana utovu wa heshima. Bwana alitaka kuzuia hilo.